Kutoka Kushoto, Wilhelm Gidabuday, Barrie na Rogart John Akhwari.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Mhe. Wilhelm Gidabuday ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya EAAR (Eastern African Athletics Region Finance Committee), ambapo makao makuu yake yapo Khartoum Sudan.

Nchi zinazounda Umoja huo ni Pamoja na Sudan, Ethiopia, South Sudan, Djibouti, Eritrea, Somalia, Kenya, Uganda, Burundi, Tanzania Bara na Zanzibar inasimama kama Taifa katika muungano huo, hivyo Kukamilisha nchi 11 za EAAR.

Wajumbe walioteuliwa ni wanne tu, ambao nchi zao zipo kwenye mabano, ni Pamoja na Wilhelm Gidabuday (Tanzania) ,Siddiq Ibrahim (Sudan), Bililign Mekoya (Ethiopia) na Peter Angwenyi (Kenya) ndipo CV ya Gidabuday ikaonekana kungara kutokana na uzoefu wake wa kuandika (Project Proposals) ambazo huwa zinasomwa hadi IAAF akachaguliwa kuiwakilisha RT kwenye Kamati hiyo.

Uteuzi huo unawaweka jumla ya Viongozi watatu wa RT katika ujumbe wa kimataifa akiwemo Rais wa Shirikisho Mhe. Anthony Mtaka ambaye ni Mjumbe wa Kamati muhimu ya IAAF na Filbert Bayi ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa EAAR.

"Pamoja na changamoto kubwa inayoikumba Shirikisho kwa sasa, watu kutoelewa kwamba focus yetu si kukimbiza kila mtu Marathon, tuna kazi kubwa ya kuwaelewesha wadau - hata wakuu wa Wizara kwamba watu kama Filbert Bayi, Bolt, Rudisha, Gatlin, Keino na mabingwa wengi wa Olympics hawajawahi kukimbia Marathon; hivyo Kilimanjaro Marathon isiwe kipimo cha mafanikio" Alisema Gidabuday.

"Pamoja na changamoto hizo lakini ninamshukuru Mungu anaweza kuleta neema ya kupata nafasi katika Kamati kubwa ya Fedha, nafasi ambayo nitaitumia vyema ili ilete tija kwa nchi wanachama kwa kuweka kipau mbele nchi yangu (Tanzania)" Aliongeza Gidabuday.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: