Leo tarehe 28 mwezi wa pili,Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,imepitisha Makadirio ya Mapato kwa Mwaka 2018/2019

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa Mwaka 2018/2019 imekadiria kutumia fefha kiasi cha Tsh 98,238,193,600 ambapo katika fedha hizo Tsh 76,607,163,700 ni matumizi ya kawaida na Mishahara ambayo sawa na asilimia 78 ya Bajeti yote na 21,631,029,900 ni fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo ambayo sawa na asilimia 22 ya bajeti yote.

Aidha Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imekidhi kigezo cha kutenga asilimia 60 ya fedha za mapato ya ndani ktk utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo ni Billioni 12 (12,600,760,400.00) na Tsh billioni 8 (8,498,717,600) sawa na asilimia 40 zimetengwa kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na Mishahara.

Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob katika Hotuba yake amesoma vipaumbele 17 vya Halmashauri kwa Mwaka 2018/2019

1. Ujenzi wa Makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Tsh Billion 3

2. Uboreshaji wa Mfumo wa Ukusanyaji Mapato ya ndani,kukusanya Tsh billioni 25.7

3. Miradi ya Maendeleo imetengewa fedha kiasi cha Tsh Billioni 21.6

4. Kuboresha utoaji wa Huduma za Afya kwa kununua madawa na Vifaa tiba Kiasi cha fedha Tsh billion 8.2 zimetengwa

5. Kupandisha Maslahi ya Wajumbe serikali za Mitaa kutoka Tsh 5000/= kwa Mwezi mpaka Tsh 20,000/=kwa Mwezi.

6. Kuboresha Miundombinu ya Barabara kwa viwango vya Lami,Matengenezo ya kawaida,kujenga madaraja na Makalvati na Vivuko vya waenda kwa Miguu, fedha kiasi cha Tsh billioni 1.4 zimetengwa kupelekwa TARURA.

7. Ujenzivwa Viwanda vidogovidogo na Uwekezaji,fedha kiasi cha Tsh billioni 1.2 zimetengwa kuanzisha viwanda vidogovidogo.

8. Mikopo ya Wanawake,Vijana na walemavu,kiasi cha fedha Tsh Billioni 1.14 zimetengwa.

9. Ukarabati wa Viwanja viwili vya Michezo na Uanzishwaji wa Meya Cup, Kiasi cha fedha Tsh 150 millioni zimetengwa.

10. Ununuzi wa Magari na Mitambo ya kisasa ya kuzolea taka na kusafisha Halmashauri,Kiasi cha fedha Tsh Billioni 1.2 zimetengwa.

11. Ujenzi wa Ofisi za walimu kwa shule za sekondary na Msingi,Kiasi cha Tsh 300 millioni zimetengwa.

12. Kuboresha Huduma za usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi,maeneo ya kwembe,kibamba,Goba,kimara,saranga,Mbezi na Msigani fedha Kiasi cha Tsh Billioni 1.303 zimetengwa kumaliza tatizo la Maji Ubungo.

13. Huduma za Afya bure kwa Wazee na upewaji wa Vitambulisho kwa ajili ya matibabu. Fedha kiasi cha Tsh 60 millioni zimetengwa.

14.kuboresha huduma za ushauri na ugani kwa ufugaji na kilimo cha mjini,fedha kiasi cha Tsh 120 millioni zimetengwa.

15.Uanzishwaji wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Ubungo,fedha kiasi cha Tsh 100 millioni kwa ajili ya utwaaji wa eneo la Hospitali na upembuzi yakinifu.

16.Uanzishwaji wa Machinjio ya kisasa ya Nyama Halamshauri ya Ubungo,fedha kiasi cha Tsh 150 Millioni zimetengwa.

17.Uanzishwaji wa Ujenzi wa Masoko makubwa ya vyakula na Nafaka, Kibamba na Kwembe fedha kiasi cha Tsh 450 million zimetengwa.

Kwa Pamoja tujenge Halmashauri yetu.

Imetolewa na Ofisi ya Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa Ubungo.
28-02-2018
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: