Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Kiwanda cha Maziwa cha The Grande Demam wakihakiki ufungashaji wa bidhaa za maziwa zinazozalishwa kiwandani hapo
Baadhi ya Viongozi wa kiwanda cha maziwa cha The Grande Demam wakinywa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho.
Baadhi ya Viongozi wa kiwanda cha maziwa cha The Grande Demam wakinywa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho.
Uongozi wa kiwanda cha maziwa cha The Grande Demam.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Wilaya ya Meru ni moja kati ya Wilaya maarufu zinazoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa maziwa mkoani Arusha,maziwa ambayo huuzwa maeneo ya miji ikiwemo viunga vya Jiji la Arusha na nje ya jiji hilo.

Licha ya uzalishaji huo wa maziwa bado wafugaji hao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko ya uhakika ya kununua maziwa hayo hivyo kupelekea maziwa wanayoyazalisha kuharibika baada ya kukaa muda bila kununuliwa.

Kufuatia Changamoto hiyo Moja kati Daktari wa Mifugo, Dokta Deo aliona changamoto hiyo kama fursa ya uwekezaji kwani malighafi ya maziwa inapatikana kwa wingi ,kwa kuwa wafugaji walikua wakiyamwaga maziwa yao yaliyokua yakiharibika kwa kukosa soko la uhakika na hawakua na namna yoyote ya kuongeza thamani maziwa hayo ili yaweze kukaa kwa muda bila kuharibika.

Dokta Deo aliacha kazi ya kuajiriwa mwaka 2001 na kuamua kufuga ng'ombe 1 baadae wawili ambao walikua wakitoa lita 40 kila siku huku yeye na familia yake wakitumia lita 1 hivyo maziwa mengine kuharibika baada ya kukaa kwa muda.

Suala hili lilimfikirisha sana Dokta Deo ambaye alimtafuta mtaalamu kutoka nchini Kenya atakayemfundisha jinsi ya kuongeza thamani maziwa yake ,kuyafungasha na kuyauza .Mtaalamu huyo alimfundisha ndipo akaianza kazi ya kuongeza thamani maziwa hayo nyumbani kwake.

Baada ya muda majirani zake wafugaji walianza kuvutiwa na jinsi anavyoongeza thamani maziwa yake na walimletea maziwa ili ayaongeze thamani ndipo alipoanza kununua maziwa na kuongeza thamani takribani lita 100,150 mpaka 200 kwa siku.

Baada ya hapo akafungua kiwanda kidogo ambacho kilikua na uwezo wa kusindika lita 200 kwa siku huku wafugaji wakileta maziwa mengi zaidi ndipo alipoongeza uzalishaji na kwa sasa anazalisha lita 2000 kwa siku.

Kutokana na ongezeko hilo lauzalishaji kwa sasa Dokta Deo pamoja na Wakurugenzi wenzake wa kiwanda hicho cha The Grande Demam wameongeza wigo na kununua maziwa zaidi kwa wafugaji ambao walikua wakiteseka kupata masoko na wakati mwingine kumwaga maziwa yao yanayoharibika kwa kukaa muda mrefu bila kununuliwa.

Kiwanda hicho kinanunua maziwa bora kutoka kwa wafugaji na kuyaongezea thamani ikiwa ni pamoja na kuyafungasha vyema.

“Maziwa ambayo hayajaongezwa thamani hukaa kwa muda wa masaa 13 lakini maziwa yaliyoongezwa thamani yanaweza kukaa hadi mwezi mmoja jambo ambalo linaleta unafuu hasa kwa kipindi kifupi kabla hayajafika sokoni” Alisema Dokta Deo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments: