Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma akifungua kikao cha Majaji wa Mahakama ya Rufani, lengo la kikao hicho cha siku moja kimelenga katika kufanya tathmini yaUtendaji kazi wa Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2017 na kuweka Mkakati na malengo ya mwaka 2018, kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T),. Benard Luanda.
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Katarina Revokati akitoa Mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliopo katika kikao cha tathmini na uwekaji wa mpango wa malengo ya utekelezaji kwa mwaka huu.
Msajili-Mahakama ya Rufani (T) akitoa Mada katika Kikao cha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani (T), katika Mada yake Mhe. Msajili amesema kuwa Mahakama ya Rufani imefanikiwa kushusha kiwango cha mlundikano kutoka asilimia 37 mwaka 2016 hadi asilimia 10 mwishoni mwa Desemba, 2017.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya ‘Oceanic’ iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Jaji Mkuu, Majaji wa Mahakama ya Rufani, Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa kwenye picha ya pamoja. (Picha na Mary Gwera).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: