Monday, March 5, 2018

MAKATIBU WAKUU 15 KUTAFUTA SULUHU ZA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI ZIWA MANYARA NA TISHIO LA KUKAUKA KWAKE

Lango Kuu la Kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara ambapo Makatibu Wakuu zaidi ya 10 kutoka Wizara mbalimbali wametembelea kujionea hali ya tishio lililopo la Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akitoa neno la ukaribisho kwa Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali katika kikao cha Mawasilisho ya Taarifa ya Tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba.
Mwenyeji wa Ziara ya Makatibu Wakuu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akifanya Wasilisho la Taarifa kuhusu tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara,Maeneo ya Shoroba na Mitawanyiko ya Wanyama Tarangire -Manyara kwa Makatibu Wakuu hao.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu hao.
Miongoni mwa Majengo yaliyokuwa yakitumika kama Vyoo katika Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara likionekana kuharibika baada ya maji ya Mvua yaliyoambatana na Mawe zilizonyesha miaka michache iliyopita.
Sehemu ya Ndege ambao ni kivutio kimojawapo kikubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ambao hutegemea pia uwepo wa Maji katika maeneo hayo ambayo kwa sasa yameanza kukauka kutokana na Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na Binadamu. Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini .

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu