Kiukweli Mwaka 2018 umekuwa ni mwaka ambao si salama kwa sisi wakazi wa Mbezi kwa Msuguli yakiwepo maeneo ya Bwaloni, Serikali ya Mtaa, Kwa Mgaya, Masaki, St. Anna, Majengo Mapya ukija mpaka Malamba Mawili Msikitini.

Nasema si SALAMA kiulinzi kwa vile huku patrol ya askari huwa ni mara moja moja sana lakini ulinzi Mwanga yani Umeme huwa ndiyo tunautegemea.

Tokea mwaka umeanza TANESCO wamekuwa wakitukatia umeme mara kwa mara kwa kisingizio kuwa line kubwa inasumbua hivyo inahitaji matengenezo sasa cha kujiuliza hiyo line huaribika kila inapofika saa 4 asubuhi naniutengemaa saa 12 jioni??? Hili ni jambo la kushangaza sana.

Baada ya wananchi wa huku kupaza sauti mmeanza tabia ya kukata umeme kila inapofika saa 6usiku na kurudisha saa 10 au 11 alfajiri jambo ambalo mnatuweka matatani hasa katika suala la ulinzi achilia mbali vitu kuharibika katika mafiriji.

Huku kwasasa matukio mengi ya wizi yamekuwa yakitokea hasa mnapozima umeme ndiyo watu wamekuwa wakivamiwa na kuibiwa mali zao maana ni giza totoro.

Ombi langu kwenu kama mmeamua kutupa mgao wa kimya kimya tutangazieni kuwa mgao upo na mtupe mgao muda ambao ni salama kwetu sisi na mali zetu muache kuchochea wizi kwa kukata mida hatarishi.

NI MIMI MWANANCHI MTIIFU,
KACHUCHU WA KACHUCHU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: