Wednesday, March 7, 2018

MDAHALO WA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI JIJINI DAR

Katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, Ubalozi wa Marekani na Kituo cha Kijinsia cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana waliandaa mdahalo wenye dhima: “Usimuache Mwanamke Nyuma” ambapo zaidi ya wanawake 300 walihudhuria mdahalo huo katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kaimu Balozi wa Marekani, Dk. Inmi Patterson, na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Bonaventure Rutinwa, walitoa hotuba za ufunguzi wakati wanawake maarufu wa Kitanzania walishiriki katika mdahalo, wakiwemo Vicky Ntetema, Mwanaharakati wa haki za kibinadamu, Joyce Mhaville, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Dk. Victoria Kisyombe, Mwanzilishi wa taasisi ya Selfina, Profesa Costancia Rugumamu, mtaalamu wa masuala ya kijinsia na maendeleo Chuo Kikuu cha Dar es Salaama, na Abella Bateyunga, mwanzilishi wa Tanzania Bora Initiatives, ambaye alikuwa mwezeshaji wa mdahalo. (Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Marekani).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu