Washiriki wa mkutano wa Wadau wa nyuki wakifuatilia mkutano kwa makini mkutano wa masuala ya nyuki uliofanyika katika chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka.Picha zote na Mahmoud Ahmad.
Washiriki wa mkutano.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa masuala ya nyuki uliofanyika katika chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka.Picha na Ferdinand Shayo

Na Mahmoud Ahmad, Kilimanjaro.

Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka kilichopo Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Wuzburg University kilichopo nchini Ujerumani wanatarajia kufanya utafiti wa nyuki ambao utasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo pamoja na uhifadhi wa mazingira.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho Ladislaus Kahana alisema kuwa kutokana na umuhimu nyuki katika uchavushaji wa mimea hivyo nyuki wanategemewa sana katika kukuza uzalishaji wa mazao .

Ladislaus alisema kuwa utafiti huo utafanyika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na baadae kufanyika katika mikoa mingine zaidi ili kuhasisha ufugaji nyuki utakaosaidia kukuza kipato na pia kusaidia shughuli za kilimo na uhifadhi.

Mratibu wa Utafiti wa Nyuki kutoka Idara ya Wanyamapori Mweka Dokta Oliver Nyakanga amesema kuwa utafiti huo ni wa miaka 3 kwa ufadhili wa Shirika la JRS Biodiversity Foundation lililoko nchini Marekani ,utafiti ambao utaangalia umuhimu wa nyuki katika kilimo ,aina mbalimbali za nyuki katika aina mbalimbali za mazingira hususan katika maeneo ya kilimo na hasa kilimo mchanganyiko.

Dokta Oliver alisema kuwa pia utafiti huo utaangalia jinsi ambavyo matumizi ya dawa na viuatilifu vinavyoathiri nyuki pia ameishauri jamii ipande miti ambayo itawavutia nyuki kukaa katika maeneo hayao kwa ajili ya uchavushaji wa maua ambayo huwa mazao.

“Tafiti nyingi ambazo hufanyika huwa ni za wanyama wakumbwa wakubwa nyuki ni wadudu muhimu waliosahaulika ndio maana kwa sasa tunakwenda kufanya utafiti ambao utatupa majibu ya uhalisia ambayo yatasaidia kuwatunza nyuki kwa ajili ya kilimo na uhifadhi” Alisema Oliver

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania Wilfred Mariale alisema kuwa kumekua na upungufu wa nyuki kwa ujumla lakini bado hakuna taarifa za kitafiti juu ya idadi ya nyuki wachavushaji,kutathmini uchavushaji katika kuboresha kilimo hivyo utafiti huo utasaidia sana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: