Mmoja wa Waandaaji wa Tamasha la Pasaka 2018, Ufoo Saro akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Tamsha hili ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha waimbaji wengine waliweza kuungana kuleta utamu zaidi ndani ya Kanda ya Ziwa na vitongoji vyake. Waimbaji waliotangazwa ni Joshua Mlelwa (Kushoto) na Mwanamama Upendo Nkone (kulia).

Ufoo Saro amesema kuwa suala la Usalam limezingatiwa vyema hivyo wajitokeze kwa wingi bila kukosa.

Katika Tamasha hilo, Mwimbaji Rose Muhando anatarajia kuzindua albamu yake ambayo amejiandaa kwa muda mrefu.

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Joseph Mlelwa (kushoto) akitoa kiburudisho cha wimbo wake wa Yesu Anaweza aliouimba mwaka 2016. Mlelwa amesema kuwa amejiandaa vyema hivyo wakazi wa Mwanza na Simiyu wajitokeze kwa ngumu ili kuweza kufanikisha zaidi tamasha hilo. Tamasha la Pasaka Mwaka 2018 litafanyika Kanda ya Ziwa ambapo Aprili 1 itakuwa ndani ya Uwanja wa CCM - Kilumba na Aprili 2, 2018 ndani ya Uwanja wa Halmashauri, Simiyu. Mwimbaji Joseph Mlelwa ni mmoja ya waimbaji wa Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group ambapo kwa sasa amekuwa akifanya kazi zake peke yake.
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone amethibitisha rasmi kushiriki Tamasha la Pasaka 2018 kwa kuwatoa hofu wakazi wa Kanda ya Ziwa wajitokeze kupata burudani ya kutosha ya kukata na shoka. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakkitambulisha mbele ya waandishi wa habari (hawapo picha) Mwimbaji huyo amesema kwa sasa amejipanga vyema hivyo wakazi wa Mwanza na Simiyu wakitokeze kwa wingi.

"Sina cha kusema zaidi ya kuwaambia wakazi wa Mwanza na Simiyu wajitokeze kwa wingi maana nimejipanga kuwapa burudani ya kutosha ikiwa ni pamoja na kumshukuru bwana kwa matendo yake makuu aliyonitendea," amesema Nkone.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: