Wakati CHADEMA ikiwa bado inafuta machozi ya kupoteza jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio mwezi uliopita, taarifa inayosambaa na kuthibitishwa inabainisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana taifa BAVICHA Getrude Ndibalema (pichani) amejiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama hicho..

Ndibalema ambaye ni mtendaji namba mbili wa BAVICHA taifa ameeleza sababu kuwa ni kutaka kujikita katika mambo binafsi yanayohusu maisha yake.

Hali hii inatafsiriwa kuwa ni kutokana na CHADEMA kupoteza muelekeo na hivyo vijana kutokua na imani na matumaini na Chama hicho.

Hivi karibuni BAVICHA ilimpoteza aliyekua Mwenyekiti wake Patrobas Katambi aliyeamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: