Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa miundombinu ya usalama barabarani katika shule za Msingi Mikumi na Mzimuni ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa uboreshaji wa usalama barababarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam ambao unaratibiwa na shirika la Amend kwa ufadhili wa Mfuko wakampuni ya Puma Energy na Mfuko wa FIA. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, walimu na maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikabidhi msaada wa jaketi la usalama barabarani kwa mwanafunzi Nuru ambae ni Muhanga wa ajali za barabarani. Nuru alilazimika kukaa hospitali kwa kipindi cha miaka miwili akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari maeneo jirani na shule hiyo.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akishirikiana na wanafunzi wenye ulemavu kutoka shule ya Gilman Rutihimaba kuimba nyimbo zenye mafunzo ya usalama barabarani.
Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, walimu na wanafunzi wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, na maofisa wa shirika la Amend, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani, walimu wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akigagua miundombinu ya usalama barabarani iliyojengwa kupitia mpango huo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: