Friday, March 9, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA ONYO KALI WA ANAYEPANGA KUANDAMANAI ILI KUVUNJA AMANI

Rais Dkt. Magufuli amesema ole wake mtu yeyote atakayeandamana siku hiyo na kama ametumwa na baba yake basi atakuja kusimulia vizuri kilichompata.

Dkt. Magufuli amesisitiza kuwa nchi hii ni ya amani na kuna watu hawapendi kuona nchi hii inaendelea kuwa na AMANI.

Ametoa rai kwa wananchi wote kuendelea kuitunza amani iliyopo kuliko kutaka kuingiza nchi kwenye migogoro kama nchi zingine tunazosikia huku mashariki ya kati na hata nchi jirani.

Rais Magufuli ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa tawi la Benki ya CRDB huko wilayani Chato leo Machi 9, 2018.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu