Tuesday, March 13, 2018

ROSE MUHANDO KUZINDUA ALBAMU YAKE YA 'USIVUNJIKE MOYO' NDANI YA TAMASHA LA PASAKA KANDA YA ZIWAMalkia wa nyimbo za Injili hapa nchini,Rose Muhando ametihitisha kushiriki tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Aprili 1 na Aprili 2 kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa maandalizi yake, Rose Muhando amesema yuko tayari kwa kazi ya kuburudisha katika tamasha hilo ambapo pia atazindua albam yake yenye jumla ya nyimbo saba, itakayojulikana kwa kwa jina la “Usivunjike Moyo” .

Katika Tamasha hilo Kiingilio kimepangwa kuwa, watu wazima ni shilingi Elfu 5000 na watoto itakuwa ni shilingi 2000 na Kiingilio katika tamasha la Pasaka mkoani Simiyu watu wazima itakuwa ni shilingi 3000 na watoto ni shilingi 2000.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu