MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wito wa kuwaita Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufika mahakamani kesho Jumatano, Machi 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo.

Taarifa za wito huo umetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole ambaye ametoa taarifa hiyo fupi kupitia kwenye ukurasa wake maalum wa Twitter.

Kambole amesema “Wito umetolewa leo (juzi Machi 19) Mahakama kuu mbele ya Jaji Samejikwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani leo 21/03/2018 kujibu kesi ya Abdul Nondo”.

Kambole amesema washitakiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa Jumatano, ni IGP Simon Sirro ameitwa kwa sababu yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini hivyo vituo vyote na polisi wapo chini yake lakini bado Nondo amekuwa hapatikani katika vituo vya polisi.

Aidha, amesema kuwa katika jalada lililofunguliwa leo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), naye kahusishwa kwa sababu mara ya mwisho Nondo alipokelewa na yeye alipofikishwa Dar es salaam kutoka Iringa na kwamba alimchukua kama muathirika wa tukio la utekwaji na siyo mshtakiwa.

Hata hivyo Kambole amesema ameshafanya jitihada nyingi za kutaka kuonana na mteja wake lakini hadi sasa juhudi zake hazijafua dafu.

Abdul Nondo anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Machi 7, ambapo awali aliripotiwa kupotea na kesho yake kujikuta Iringa.

Baadaye alisafirishwa hadi Dar kwa ajili ya upelelezi zaidi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari alisema wanamshikilia Nondo kwa ajili ya upelelezi na watakapokamilisha watamfikisha mahakamani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: