Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake (cryotherapy machine). Anayeshuhudia kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt Asha Mahita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya makabidhiano hayo (kushoto) ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt Asha Mahita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa (katikati) akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Monica Kinala
---
SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake (cryotherapy machine).

Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa
wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika vifaa tiba.

"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii  ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu  katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema  Mwakyusa.

Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru  shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza  atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza (Muheza DDH) ili ianze  kazi.

Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia  kifaa hiki muhimu kwa wakina mama, nikisema kikae mpaka hospitali  ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.

Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya  alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo.

(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: