Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa Meneja wa Kanda wa Nchi za Afrika zilizo Jangwa la Sahara wa Kampuni ya Progress Rail Caterpillar, Barend Hanekom wakibadilishana mikataba mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano.
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa Meneja wa Kanda wa Nchi za Afrika zilizo Jangwa la Sahara wa Kampuni ya Progress Rail Caterpillar, Barend Hanekom wakionesha mikataba kwa waandishi habari mara baada ya kusaini jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.

Shirika la Reli Nchini (TRC) limeingia mkataba wa ununuzi vichwa vya trein 11 na kampuni ya Progress Rail Locomotives (PRL) ya Marekani ili kuweza kuongeza idadi ya vichwa katika shirika hilo

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Masanja Kadogosa amesema kuwa ununuzi wa vichwa hivyo itafanya shirika kuwa vichwa 47.

Amesema walikuwa na vichwa 29 ambavyo kwa mahitaji vilikuwa havitoshi lakini kwa sasa shirika linatakuwa vichwa vya kutosha katika kutoa huduma nzuri kwa wateja wa TreinI.

Amesema kuwa vichwa vitafanya majaribio katika awamu tatu ambapo ya kwanza ni kuangaliwa na watalaam katika ubora wake na awamu nyingine kuviwasha na kupakia tani 700 toka Dar es Salaam pamoja na hatua ya tatu kupakia tani 1200 toka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.

Kadogosa amesema serikali imeokoa zaidi dola 8,800,000 kwa kila kichwa kutoka dola 3 200,000 kutokana na na mazungumzo ya kamati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: