Na Kibena Kindibwa - Uganda.

Redio 23 hazitakuwa hewani Uganda Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) imesitisha leseni za vituo 23 vya redio kwa tuhuma za kushabikia na kueneza uchawi.

Kwa mujibu wa msemaji wa tume hiyo, bi Pamela Ankunda, redio hizo zimekuwa zikihusika katika kukuza uchawi kwa njia ya kutoa matangazo (witchcraft content) ya uchawi. Redio hizo ni Metro FM, Nile FM, Kagadi Broadcasting Services, Emambya FM, Village Club FM, Radio Kitara, Packwach FM na Tropical FM.

Nyingine ni Apex FM, Bamboo FM, Ssebo FM, Eastern Voice FM, Eye FM, Victoria FM, RFM, Kiira FM, Tiger FM, Greater African Radio, Dana FM, Gold FM, Hits FM na Radio 5.

Kifungu cha 41 (1 a &b) cha Sheria ya Mawasiliano Uganda ya Mwaka 2013, kinatoa jukumu kwa tume hiyo kusitisha au kufuta leseni ya chombo chochote cha habari nchini humo ambacho kinakiuka masharti ya leseni husika.

Bi Ankunda amesema vituo hivyo vya redio viwahi kuonywa kuhusu mwenendo wao kabla ya hatua hiyo ya kuvifungia.

Anasema walivionya vituo hivyo kwa kukiuka matakwa ya utangazaji yaliyowekwa na UCC.

Alisema redio hizo zitaruhusiwa kurejea hewani kama wahusika wataahidi kwa maandishi kufuata masharti ya leseni zao, na kamwe hawatangaza masuala ya uchawi au kujihusisha na shughuli zozote ambazo kwa namna moja au nyingine zitahusiana na ufisadi wa kieletroniki.

Amezishauri redio hizo kuwapa mafunzo watangazaji wake kuhusu mambo gani yanaruhusiwa na mambo gani hayaruhusiwi wakati wa kutangaza ili kujiepusha na makosa kama hayo siku za baadaye.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: