Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika, sehemu ya vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti, vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma. Wengine pichani ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Hospitali hiyo, Neema Tawale (wa pili kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Huduma za Uuguzi, Salome Kasanga.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akieleza jambo kwa waandishi wa habari juu ya vifaa hivyo vilivyogharimu dola za Marekani elfu ishirini (20,000 USD) huku Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (kulia) wakimsikiliza, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem, Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt.  Alphonce Chandika wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Januarius Hingi wakati akitoa maelezo ya namna vifaa hivyo vitakavyosaidia wakina mama wanaojifungua watoto wanaozaliwa kawaida na wale wanaozaliwa kabla ya wakati.
Sehemu ya vifaa hivyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: