Muwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez.
Muwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa Simba katika Kituo cha Kimataifa AICC Jijiji Arusha.

Na Vero Ignatus, Arusha.

Umoja wa mataifa umekubali kuingia makubaliano na Serikali ya Tanzania kupitia chama cha maafisa habari na mawasiliano na wa Serikali na uhusiani TAGCO katika sekta ya habari ambapo mkataba huo utatoa nafasi kwa wanahabari kutembelea na kuitangaza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.

Muwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez amesema UN ni mshiriki mwenza wa maswala ya maendeleo kwahiyo kwao mkutano kama huo ni muhimu ambapo shirika la maendeleo la umoja wa Kimataifa (UNDP) ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa malengo ya dunia kwa miaka miwili iliopita ili kufanikisha malengo hayo kwa miaka 13 ijayo.

Amesema kuwa Umoja wa Mataifa kupitia wanamawasiliano wake kwa kushirikiana na serikali wanaweza kuijua Tanzania ya viwanda Tanzania ya maendeleo ,hivyo basi wataonyesha matokeo chanya yanayofanywa na serikali ambapo wapo tayari kufanikisha malengo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti chama cha maafisa wa habari na mawasilianao na uhusiano serikalini Pascal Shelutete amesema kusainiwa kwa mkataba huo kutatoa fursa ya malengo yaliopo baina ya serikali ya Tanzania na umoja wa mataifa yanatekelezwa kwa wakati huku.

Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo ambapo pia ni msemaji mkuu wa serikali Dkt. Hasan Abbas amesema mkataba huo na utawawezesha maafisa habari kutekeleza kwa haraka malengo 17 ya milenia.

Dkt. Abbas amesema kuwa kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa inaandaaa mradi wa maendeleo inayotekelezwa chini ya malengo ya mileniamu

Amesema hata hivyo wapo katika hatua za awali a mazungumzo na shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ambapo mradi huo utakuwa na manufaa kwa waandishi wa habari na serikali itaona ile miradi ambayo ilikuwa haijulikani na wananchi sasa itaonekana kwa ushirikiano huu utaibua miradi hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: