Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akizungumza na Wajumbe Wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Kigamboni, alipofanya ziara ya Kikazi katika Wilaya hiyo na Temeke, leo. Dorothy ambaye alifuatana na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa huo, amesisitiza kuwa ni lazima viongozi watambue kuwa muda wa maandalizi ya ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao ni sasa.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga akizungumza wakati wa kikao cha Kazi kati ya Mwenyekiti wa UWT mkoa huo na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT Wilaya ya Kigamboni, leo. Malyaga amesema UWT mkoa wa Dar es Salaam, Wanampongeza Rais Dk. John Magufuli kwa uthubutu aliofanya mwishoni mwa wiki iliyopita, kukutana na kufanya mazungumzo ya kina na Wafanyabiashara mbalimbali hapa nchini. "Sisi tunaaamini hatua hii itasaidia sana kuondoa au kupunguza changamoto zinazonyemelea sekta ya biashara nchini", alisema Tatu Malyaga.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akiongozana na Wabumbe wa Baraza la Utekelezaji la mkoa huo, kuingia ukumbini wakati wa kikao hicho cha kazi Kigamboni. Kulia ni Wajumbe hao, Elizabeth Lameck na Hawa Nguh'umbi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigamboni Agnes Seng'unda akimwongoza Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga kwenda ukumbini. Kulia ni Katibu wa UWT Kigamboni Nasma Abdallah
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigamboni Agnes Seng'unda akizungumza mwanzoni mwa kikao hicho cha kazi.
Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la UWT mkoa wa dar es Salaam, Elizabeth Lameck akisalimia baada ya kutambulishwa na Malyaga.
Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam Hawa Nguh'umbi akisalimia baada ya kutambulishwa.
Washiriki wa kikao hicho cha kazi wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave, Katibu wa UWT mkoa huo Tatu Malyaga na Wajumbe wa Baraza la Utekelezaji la UWT mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho cha kazi.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave akipewa chakula na mhudumu, wakati wa chakula cha mchana baada ya kikao hicho cha kazi
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Tatu Malyaga akipewa chakula na mhudumu, wakati wa chakula cha mchana baada ya kikao hicho cha kazi
Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Lameck akipewa chakula na mhudumu, wakati wa chakula cha mchana baada ya kikao hicho cha kazi
Baadhi ya viongozi na washiriki wa kikao hicho cha kazi wakipata chakula. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UWT mkoa wa Dar es Salaam Hawa Ngh'umbi.
Baadhi ya viongozi na washiriki wa kikao hicho cha kazi wakiwa kwenye foleni ya chakula.
Baadhi ya viongozi wa UWT Wilaya ya Kigamboni wakipata chakula.
TEMEKE:
Ujumbe ukiingia ukumibi.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Dorothy Kilave akisaini kitabu cha wageni.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Malyaga akisaini kitabu cha wageni.
Hawa Ngh'umbi akisaini kitabu cha wageni
Elizabeth Lameck akisaini kitabu cha wageni. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: