Kaimu Mkurugenzi ufatiliaji na Tathimini wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) Dkt. Annastella Sigwejo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua walizozichukua kwa vyuo vya ufundi vinavyoendedha mafunzo bila sifa leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkuu wa kitengo cha Udahili kutoka (NACTE),Twaha Twaha.
Mkuu wa kitengo cha Udahili wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) (NACTE),Twaha Twaha akizungumza kuhusiana na udahili wa Stashahada na Astashahada ulionza machi na kuishia Aprili 25 leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi ufatiliaji na Tathimini wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) Dkt. Annastella Sigwejo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) imevizuia vyuo 163 nchini kutofanya udahili kwa wanafunzi mwaka huu baada ya kubainika vyuo hivyo vina kosoro mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi ufatiliaji na Tathimini kutoka (NACTE) Dkt. Annastella Sigwejo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema Nacte ilifanya ufatiliaji wa kuangalia ubora wa vyuo mbali mbali vilivyosajiliwa na Baraza hilo.

Amesema katika kufutia huo walivikagaua vyuo 459 ambapo vikabainika vyuo 290 tu ndio vilivyokidhi vigezo vya kufanya udahili wa wanafunzi kujiunga navyo huko vyuo 163 vikawa vinakosoro mbali mbali ambapo haviwezi kuendelea kufanya udahili.

Dkt Sigwejo ametaja baadhi ya kasoro hizo ni kutokuwa na watalamu wenye sifa za kufundisha ,kutokuwa na miundomibinu lafiki ya kufundishia.

Hata hivyo, Dkt Sigwejo amewataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo ambavyo vina sifa wanakatiwa kuangalia kwenye mtandao wa Baraza hilo (WWW.NACTE.GO.TZ) ambapo amefafanua huko kutakuwa na oradha ya vyuo vyenye sifa pamoja na kitabu ambacho kitatoa mwongozo wa mwanafunzi kuelewa kwa undani chuo na kozi anayotaka kuisomea.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Udahili kutoka (NACTE),Twaha Twaha amesema zoezi la udahili kwa wanafunzi wa Stashahada na Astashahada mbalimbali ambapo zoezi hilo limesha aanza tangu Februari ,2018 hadi Marchi 25 mwaka huu.

Twaha amesema katika udahili huo kozi za Afya udahili waka mwisho utakuwa 10 Aprili mwaka huu.Ambapo udahili hauhusishi kazo za Afya katika vyuo vya serikali ambapo udahili wake unafanywa na wizara ya Afya,Maendeleo Jinsia na Watoto ambapo wanadhamana ya kufanya udahili katika vyuo vya afya vya serikali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: