Wednesday, March 7, 2018

WAFANYAKAZI TBL WALIVYOSHIRIKI KILIMANJARO MARATHON 2018

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakipongezana baada ya kumalizika mashindano ya Kili Marathon 2018.
Moja ya vibanda vyenye vipeperushi vya kampeni ya kupanda miti na maelezo vilivyokuwa vimewekwa mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi.

Idadi kubwa ya wafanyakazi kutoka kampuni ya TBL Group wameshiriki mbio za Kili Marathon zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.Mashindano haya maarufu duniani yanadhaminiwa na kampuni hiyo kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premier Lager.

Mwaka huu TBL Group imekuja na ajenda ya kuwezesha na kuhamasisha upandaji mti katika maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro ili kulinda mazingira,ambapo kwa kushirikiana na taasisi ya Kilimanjaro Project, inatarajia kupanda miti 100,000.

Uhamasishaji wa mradi huu umeanza kutekelezwa wakati wa mashindano ya Kili Marathon yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu