Wapalestina 15 wamekufa shahidi na wengine zaidi ya 1,416 wamejeruhiwa jana Ijumaa, kufuatia kupigwa risasi na kukosa pumzi katika mapigano na majeshi ya kivamizi ya Israeli na walenga shabaha, yaliyotokea kwenye mistari ya mpaka wa kaskazini mashariki mwa Ukanda wa Gaza.


Baada ya Wapalestina kushiriki katika maandamano ya amani (kuadhimisha miaka 42 ya Siku ya Ardhi) katika Ukngo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, isipokuwa utawala wa kivamizi wa Israeli ulikabiliana na maandamano haya kwa unyama wa hali ya juu,pale ilipowapiga risasi waandamanaji hao na kupelekea kuuawa kwa idadi hii kubwa ya Wapalestina.

Rais wa Dola ya Palestina “Mahmoud Abbas” ameubebesha utawala huo wa kivamizi wa Israeli jukumu kamili la mauaji hayo ya jana, pia majeruhi kufuatia hatua ya jeshi lake kuyakabili kwa risasi maandamano ya amani ya kitaifa, yaliyotoka kwa lengo la kuadhimisha siku hii na kushikamana na haki yake katika kujiamulia mustakabali wake kama ilivyo kwa mataifa mengine ya dunia.

 Katika hotuba yake jana Ijumaa, Rais aliomba Umoja wa Mataifa kufanya haraka kutoa ulinzi wa kimataifa kwa wananchi wa Palestina wasio na mtetezi, kutokana na uadui huu wa kila siku unaoendelea na kuzidi. 


Rais ameongeza kusema kuwa,”Hakika kuuawa kwa idadi hii kubwa ya mashahidi pia kujeruhiwa kwa wengine katika maandamano ya amani ya kitaifa, kunatilia mkazo wajibu wa jamii ya kimataifa wa kutoa ulinzi kwa wananchi wetu wa Palestina wasio na mtetezi”.

Aidha Rais Abbas ametangaza kuwa leo jumamosi ni siku ya maombolezo ya kitaifa kwa roho za mashahidi hao, ambao waliouawa jana kwa risasi za majeshi ya Israeli.

Matukio ya Siku ya Ardhi ya Wapalestina yanaanzia mwaka 1976, baada ya utawala wa kibaguzi wa Israeli kuchukua kwa mabavu maelfu ya Dunum (ekari) ya ardhi ya Kiarabu zenye umiliki binafsi au wa jumuiya, ndani ya mipaka ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu, chini ya kivuli cha amri mpya iliyotolewa katikati ya miaka ya 1970 iliyojulikana kama "Maendeleo ya Jalil",huku msingi wake hasa ukiwa ni "Kuingiza uyahudi Jalil". 

Hivyo, imekuwa sababu ya moja kwa moja ya matukio ya siku ya ardhi, ni kitendo cha utawala wa kizayuni kuchukua kwa mabavu dunums 21,000 za ardhi ya Araba, Sakhnin, Deir Hanna na Sawa'ad ya Kiarabu na zingine zilizopo katika maeneo ya Jalil nchini Palestina iliyokaliwa kwa mabavu mwaka 48 (navyo ni vijiji viavyojulikana leo kwa jina la Pembe tatu za Ardhi).


Na kutengwa maeneo hayo kuwa ni rasmi kwa makazi ya kizayuni,katika mazingira ya mpango wa kuingiza uyahudi mjini Jalil,huku ikijulikana kwamba utawala wa kizayuni tayari umeshachukua kwa mabavu zaidi ya ekari milioni kati ya miaka ya 48-72, ikiwa ni miongoni mwa ardhi ya vijiji vya kiarabu mjini Jalil na eneo la pembe tatu, pamoja na mamilioni ya Dunum zingine ilizochukua mwaka 48 (Navyo ndivyo vijiji vinavyojulikana leo kama Pembe tatu za ardhi). 

Kufuatia mpango huu wa kibaguzi, mnamo tarehe 1/2/1976 Kamati ya Ulinzi wa Ardhi iliamua kufanya mkutano wake mjini Nazareti, kwa kushirikiana na Kamati ya Qarari ya Wakuu wa Mabaraza ya Kiarabu na kufikia azimio la mgomo wa jumla tarehe 30 Machi,ikiwa ni kupinga sera ya uchukuaji ardhi kwa mabavu.

Hatimae kama kawaida ilivyo, majibu ya jeshi la Israeli yalikuwa ni umwagaji wa damu,pale lilipovamia vijiji vya Palestina na miji ya kiarabu huku yakiwa na vifaru na magari mengine ya silaha na kuanza kupiga risasi ovyo na kupelekea kufa shahidi “Khair Yassin” kutoka kijiji cha Araba. Baada ya habari kuenea asubuhi ya siku iliyofuata Machi 30, raia walifanya maandamano makubwa na kupelekea vifo vya mashahidi wengine watano na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Tokea tarehe hiyo kila mwaka, Wapalestina wote walio katika ardhi iliyovamiwa kimabavu mwaka 1948, iwe Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza au maeneo mengine, wanaadhimisha Siku ya Ardhi wakitilia mshikamano wao katika ardhi yao, pia kuendeleza mapambano yao kwa lengo la kurudishwa haki iliyoporwa kwa wamiliki wake wa kisheria.

Aidha maadhimisho ya 42 ya Siku ya Ardhi, yanakuja katika nyakati za hatari zinazokabili suala la Palestina ili kulisitisha,hayo yanatokana na tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Jerusalem ni mji mkuu wa Israel tu na kwamba ubalozi wa Marekani utahamia mjini Yerusalemu pamoja na kupinga kwa Umoja wa Mataifa na nchi nyingi duniani, kwani hatua hiyo inazingatiwa kuwa na lengo la kubomoa ufumbuzi wa dola mbili katika Mashariki ya kati. 

Hilo limepelekea vikundi vyote vya kitaifa na kiislamu nchini Palestina pamoja na wananchi wote, kuandamana ili kuonesha kushikamana kwao na haki yao pia kutokubaliana kwao na matendp yote ya kivamizi ya Israeli, yanayolenga watu, mawe,miti na kila kitu nchini Palestina.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: