Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa suti) akimkabidhi bendera Kapteni wa Timu ya Taifa ya Tenisi Bw.Masoud Mtalaso leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya timu zote za michezo zinazoondoka nchini kesho jioni kwenda katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayofanyika nchini Australia katika mji wa Gold Coast.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wanamichezo wanaokwenda katika mshindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia na kuwataka wawe wazalendo na kutangaza utalii wa nchi leo jijini Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi bendera ya Taifa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Olimpiki nchini pamoja na wachezaji wanaokwenda katika mashindano ya Jumuiya ya Madola katika sherehe ya kukabidhi bendera kwa wanamichezo hao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, wa kwanza kushoto ni Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Rashid Gullam na wapili kulia ni Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Filbert Bayi. Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: