Washindi wa wiki ya nne katika picha ya pamoja
Washindi wa pikipiki wakifurahi baada ya kukabidhiwazawadi zao.
Baadhi ya washindi wakisubiri kupokea zawadi katika hafla hiyo.

Wakati promosheni ya mzuka wa Soka na Coka imeingia katika wiki ya 4 tangu izinduliwe ,zaidi ya wakazi 32 wa mikoa ya, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida wamejishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa za pikipiki,Luninga bapa za kisasa na fedha taslimu shilingi 100,000/-

Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kubwa kwa washindi wa wiki ya nne,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Bonite Bottlers, Chris Loiruk,alisema

kumekuwa na ongezeko la washindi katika wiki ya nne tangu kuanza kwa promosheni hiyo,na kampuni inayo furaha kuona wateja wake wanaendelea kushiriki katika promosheni hii na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali.

“Zipo zawadi nyingi zimeandaliwa kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha taslimu kuanzia 5,000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito waendelee kushiriki waweze kujishindia”,Alisema Loiruk.

Washindi wapatao 18 ambao walikabidhiwa zawadi zao za Pikipiki,Luninga na Fedha taslimu katika hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite mwishoni mwa wiki waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuwakwamua wateja wake kiuchumi.

Akiongea kwa niaba ya washindi waliokabidhiwa luninga, Denis Stanslaus mkazi wa Rau Madukani, Manispaa ya Moshi,alisema wamefurahi kupata zawadi za luninga za kisasa hususani katika kipindi hiki kuelekea mashindano ya kombe la dunia kwa kuwa wataburudika na mashindano hayo na familia zao na kupata habari kupitia luninga bapa za kisasa.

Akiongea kwa niaba ya washindi wa pikipiki, Jackline Emmanuel, mkazi wa Kijenge Juu Mkoa wa Arusha ,alisema kuwa wanayo furaha kubwa kwa zawadi waliyojishindia na chombo hicho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha usafiri sambamba na matumizi ya biashara kwa ajili ya kuongeza pato la familia.

Kwa upande wake, Elinaisha Nasari , Mkazi wa Tengeru Mkoa wa Arusha , akiongea kwa niaba ya washindi wa fedha taslimu shilingi 100,000/-alisema kuwa fedha walizojishindia zitawawezesha kutatua matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakiwakabili sambamba na kuongeza mitaji yao ya biashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: