Beki wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 na timu ya Mtibwa Sugar, Dickson Job amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom.

Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur amesema kuwa katika kusaini mkataba huo mpya Job alikuwa Sambamba na kaka yake anayetambulika kwa jina George Job kwa sababu yeye mwenyewe hajafikisha umri wa miaka 18.

Swabur amesema kuwa hii ni kawaida kwa timu yao kuwa na vijana wengi sana na hasa ukizingatia waliweza kuwa na Job kwaa muda kidogo kwahiyo wameonelea bora wampe mkataba kamili kwa ajili ya kuwa nae katika kupindi hiki ili awezw kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Ameendelea kusema kuwa Mtibwa Sugar inaendeleza sera zake za kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi nchini kwa kumpa mkataba mzuri Job.

“Huu ndiyo umekuwa utamaduni wa Mtibwa kwa miaka mingi, kuchukua wachezaji wakiwa vijana wadogo na kuja kuuwalea huku. Nasi tunaahidi kuuendeleza, hatutaishia hapa Kwa Job tu, hivi karibuni mtasikia zaidi,”alisema Swabur.

Kwaa upande wa mchezaji mwenyewe, Job amesema kuwa amefurahi kuongeza mkataba na wakata miwa hao wa manungu cha zaidi anaahidi kufanya kazi ili aweza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwani anaamini ana uwezo huo.

Job alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika (AFCON U17) nchini Gabon Mei mwaka jana na kwa sasa amepandishwa kwenye kikosi cha U20, Ngorongoro kinachoshiriki mechi za kufuzu AFCON U20 mwakani nchini Niger.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: