Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwaunga mkono wajumbe waliokuwa wakimshangilia baada ya kuwasili ukumbini kwenye Kongamano la miaka 63 ya kuzaliwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoandaiwa na Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa dar es Salaam Frank Kamugisha.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwa na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, tayari kushiriki kongamano hilo
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Mwinyimkuu Sangaraza akifungua pazia la kongamano hilo kwa kufanya utambulisho
"Jamani sare maalum ya sherehe hizi ilichelewa kidooogo, lakini ninayo imeshafika hii hapa" akasema Sangaraza na kuwaacha wajumbe na mgeni rasmi wakicheka
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala akisalimia baada ya kutambulishwa.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam wakisalimia baada ya ktambulishwa. Kutoka Kushoto ni Katibu wa Uchumi na Fedha habib Nasser, Mwafongo na Kamugisha.
Wazee wa Jumuiya ya Umoja wa wazazi mkoa wa Dar es Salaam (mstari wa mbele) wakiwa kwenye kongamano hilo.
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo akizungumza kwenye kongamano hilo.
Wajumbe wakimshangilia Mwanfongo wakati akifanya utambulisho
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Jumiya ya Umoja huo Mzee Mkali akisalimia baada ya kutambulishwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha akitoa nafasi ya kufanywa dua na maombi kabla ya kongamano kuanza rasmi
Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akiomba dua kabla ya kongamano kuanza.
Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akiomba dua kabla ya kongamano kuanza.
Wajumbe wakipokea dua ya Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) kabla ya kongamano kuanza.
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira wa Jumiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Wilson Tobola akisoma maombi kabla ya kongamano hilo kuanza
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo akisoma taarifa ya maadhimisho ya miaka 63 ya Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania wakati wa Kongamano hilo.
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo akimkabdhi taarifa hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo baada ya kuisoma. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: