MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo jijini humo kuhusu upokeo na maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi,ndani ya uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo kwenye moja ya hoteli jijini humo, akieleza kukamilika rasmi kwa maandalizi ya tamasha la pasaka,linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

Msama amewashukuru Maaskofu hao na Wachungaji kwa kujitoa na kuunga mkono Tamasha la Pasaka 2018,ambalo kwa mara ya kwanza linaanzia kufanyika jijini Mwanza na baadae kuhamia mkoa wa Simiyu ndani ya mji wa Bariadi April 2 ndani ya uwanja wa Halmashauri,aidha tamasha hilo litakuwa na waimbaji lukuki ambao tayari wameishatangazwa kushiriki,kuhakikisha tamasha hilo linafana.

Kwa upande wa Maaskofu wameipongeza Kampuni ya Msama Promotions,chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama kwa kuupa mkoa wa Mwanza kipaumbele kwa kuleta tamasha hilo mkoani humo,Wameongeza kuwa tamasha hilo litawavuta waumini wengi na wapenzi wa muziki wa injili na kuwaleta pamoja ili kupata neno la mungu na uponyaji kwa njia ya uinjilisti wa nyimbo za injili.

Katika picha kutoka kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza na Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa Msama Promotion Kanda ya Ziwa.
Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa kampuni ya Msama Promotion Kanda ya Ziwa,akitoa ufafanuzi wa namna tamasha hilo la Pasaka 2018 lilipofikia na maandalizi yake kwa ujumla, mbele ya kikao cha Maaskofu na Wachungaji kilichofanyika mapema leo jijini humo,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza.
Mmoja wa maaskofu akitoa mchango wake katika kikao hicho kilichofanyika jijini Mwanza leo.
Askofu Joyce Mangu wa kanisa la Calvary Assemblies Of God Mjini Kati jijini Mwanza akizungumza wakati akitoa mchango wake katika kuboresha tamasha hilo siku za usoni na kwamba amefurahishwa sana na ujio wa tamasha hilo kwa jiji la Mwanza.
Baadhi ya maaskofu na wachungaji wakifuatilia kikao hicho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: