Umemuomba akutumie picha ya utupu.
Akakuambia siwezi nauheshimu mwili wangu siwezi kufanya hicho kitu.
Ukambembeleza na kumsihi kwa maneno matamu yenye ulaghai.
Bado akakuambia kwamba anajipenda na kukupenda pia hawezi kufanya kitu kama hicho, akakuambia kama unashida ya kuonana nae vumilia usiku huo sio mbali kesho atakuja tena akutembelee.
Ukamng'anganiza na kujifanya umechukia na kama vipi muachane nae.

Mtoto wa watu kwakuwa anakupenda na hataki kuachana na wewe akakuambia subiri kidogo, akainuka kitandani na kuvua nguo zake.
Akachukua simu yake na kujipiga picha moja kisha akakutumia.
Ukamshukuru na kufurahi kuuona mwili wake.
Mwili ukakusisimka kwa kumtazama kisha ukaanza kumsifia kwamba ameumbika.
Baada ya kumwagia sifa za uongo ambazo hazitoki moyoni kweli sasa ukaona ni wakati wa kumchafua.

Ukatoka whatsapp ambako mlikuwa mnachart nae moja kwa moja ukaingia Fb.
Bila hata aibu ukaiingiza picha yake kwenye akaunti yako na kuipost katika ukurasa wako.
Baadhi ya watu walikulaumu kwa kile ulichokifanya, wengine wakakusifia kwa kupata msichana mwenye umbo zuri, wengine wakaidownload picha hiyo na kuzidi kuisambaza. Binti wa watu anaamka asubuhi anakutana na sms za marafiki zake wakimpa taarifa kwa kile kinachoendelea kwenye akaunti yako.

Anaingia kwenye ukurasa wako anakutana na picha yake aliokutumia jana usiku.
Watu wamekoment kwa kumtukana na kujidhalilisha, wapumbavu wengine wamemsifia.
Binti wa watu anakupigia simu huku analia.
Anakuomba uifute hiyo picha lakini unagoma.
Anakuomba na kusema uifute hiyo kama unataka zingine atakutumia lakini hiyo picha ifute bado unagoma.
Unamjibu kwamba sina shida na hizo picha zingine kwasababu kwenye hiyo picha umeshaona kila kitu.

Binti wa watu anakosa raha, anabaki analia.
Anajaribu kutoka nje kuendelea na shughuli zake.
Anapita mtaani kila mtu anamnyooshea kidole.
Picha imeshazagaa kila sehemu, watu wameshaipost na kuisambaza karibuni mitandao yote ya kijamii.
Binti wa watu kila atakakopita ni aibu tu, anaonekana kama yupo uchi.

Wakati wa shule unafika.
Anaenda shule kwa ajili ya kuendelea na masomo.
Maskini wanafunzi mpaka waalimu wake nao wameshapata picha yake.
Kila atakakopita wanamnyooshea vidole na kumcheka.
Hatimae wazazi wanaitwa shule na mkuu wa shule.

Wanaelezwa hali halisi iliyopo kisha mkuu wa shule anachukua uamuzi wa kumfukuza binti wa watu shule.
Wazazi wanaomba msamaha kwa mkuu wa shule wanapiga magoti na kulia lakini mkuu ameshatoa maamuzi.

Wazazi wanakosa la kufanya zaidi wanamchukua binti yao na kurudi nae nyumbani.
Kila kona na kila mtaa ni aibu kwa binti.
Vicheko na maneno ya kejeli vimejaa kila sehemu apitayo.
Binti anaamua anunue sumu ya panya.
Anajifungia chumbani kwake kisha anakunywa.
Muda si mwingi povu linamtoka mdomoni.
Hatimae bila kuchelewa roho inaacha mwili.
Anaamua ajiue ili kukimbia aibu na maumivu anayoyaona.

Wazazi wanamtafuta aliko na hatimae wanakuja kumkuta chumbani kwake wakati huo ameakauka na kukauka.
Kilio kwa wazazi kinatawala.
Kilio kwa marafiki kinatawala.
kilio kwa mtaa kinatawala.
kilio shuleni kinatawala.
Wote wanamlilia binti.
Hatimae siku ya mazishi inafika.
Umati wa watu umezunguuka nyumbani kwa binti kutoa heshima zao za mwisho.
Wewe kwa mbali ukiwa msibani unashuhudia jeneza lake limewekwa katikati ya watu.
Moyo unakusuta kuwa wewe umesababisha umauti wa binti huyo.Chozi la aibu linakutoka eti unamlilia mpenzi wako.
Hatimae watu wanauchukua mwili tayari kwa ajiri ya mazishi rasmi.

MASKINI ndoto na historia ya binti huyo inakuwa imeishia hapo.

UJUMBE:

BINTI heshimu mwili wako. Ufanye kama sehemu takatifu iliyobarikiwa na Mungu. Hata kama ni mpenzi wako au Mume wako ni lazima awe na mipaka na mwili wako na si aufanye kama wake.

Wakumbushe Mabinti wengine japo kwa ku-share.Ukimfindisha tabia njema mwanamke ujue umeifundisha Dunia maana Asilimia 75 ya malezi na mafunzo hutoka kwa Mama.

MBARIKIWE KAMA NIMEELEWEKA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: