Kumbukumbu: Mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto barani Africa Graca Machel (kulia) akiwa na mke mwenzake marehemu Mama Graca Machel.

Na Leah Mushi (GMT - Tanzania)

Mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto barani Africa Graca Machel ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Winnie Mandela.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mama Graca amesema Marehemu Winnie Mandela (81) alikuwa mwanamke shupavu wa kupigiwa mfano na ambaye alihamasisha wengi katika kupigania haki na usawa katika jamii.

“Maisha yake ya ajabu na kipekee yaliyojaa changamoto na harakati yamekuwa kivutio na hamasa kwa watu wengi katika jamii chakuonesha jinsi ya kujipa moyo, kutokata tamaa pindi tunapokumbwa na changamoto huku tukiwa na matumaini ya kwamba tutafanikiwa” amesema Graca Machel.

Ameongeza kuwa Marehemu Winnie Mandela kwake ni dada mkubwa ambaye amekuwa akipendwa wa watu si wa Afrika Kusini pekee bali duniani kote kwa ujumla kutokana na Upendo wake na kujitoa kupigania ukombozi wa taifa hilo.

Pamoja na kupita katika kipindi hiki cha machungu na huzuni ya kumpoteza mpendwa wao Mama Graca amewasihi wote walioguswa na msiba huo kujiimarisha na kuendelea kutetea haki za raia katika jamii zinazowazunguka kwani kwa kutenda hivyo watakuwa wakimuenzi Winnie Mandela

Graca Machel ni nani:

Graca Machel ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake na watoto barani Afrika. Kupitia harakati hizo amekua mwanzilishi wa Wakfu wa Graca Machel ( Graca Machel Trust- GMT).

Kupitia wakfu huo Mama Graca Machel ameweza kuanzisha mtandao wa Wanawake Afrika katika masuala ya Uwekezaji na uwezeshaji kiuchumi, afya ya mama na mtoto,, kilimo biashara na mtandao wa wanahabari.

Mama Machel alikuwa mke wa Marehemu Nelson Mandela baada ya kuachana na Marehemu Winnie Mandela ( 1998- 2013) makazi yake ni Johannesburg Afrika Kusini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: