Nimekuwa nikiishi nje mda mrefu sana nikiona kaka zangu wakioa wazungu na nikisema kaka zangu i mean africans.

Kinachonishangaza ni kwamba mtawaabudu wake zenu wa kizungu kwa kutowapiga, kutowanyanyasa, kuwanusa mpaka makwapa, lakini dada zenu waafrika wenzenu mtawafanyia vituko na kuwatesa juu kisa tu uonyeshwe wewe ndio mwanaume wewe ndio kichwa cha familia.Sasa utakuwaje kichwa cha familia wakati umeletwa, unalelewa, unatunzwa, unahifadhiwa na mtu ambaye kakuona na kakupenda na akataka upate maisha bora ila wewe unatake advantage yakutaka bado usujudiwe.

Mbona mkiletwa na makaburu mnanyooka, mna adabu na kuufyata lakini dada zenu oooh! hao mnataka muwapande kichwani, SHAME ON YOU.

Sishangai baadhi ya wanaume kumtetea muuaji wa Leyla tena mbele ya mtoto wake wa kike kwa kumpiga na kumdhalilisha then kumuua kwa kumchoma kisu zaidi ya mara kumi... sishangai maana hakuna mtesaji wa wanawake wa kiafrika kama mwafrika kubalini kataeni huo ndiyo ukweli.

Niliandika while back kuwa nimegundua kwanini mwafrika aliweza kutawaliwa but nimegundua pia kuwa MWANAMKE wa kiafrika ana safari ndefu sana KUTHAMINIKA si nje tu bali hata NYUMBANI KWAKE AFRIKA.

Kifo cha Leyla kiwe somo na fundisho kwa wengine na Mjitizame na kuwa makini na nani? unayemleta ndani ya moyo wako na mwisho wa siku mkashare the same bed, Rest In Peace Leyla!

Ni Mimi,
Nuru Light.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: