Ndugu msomaji naomba uniruhusu nianze na msemo wa Wahenga :

" USIONE VYAELEA, VIMEUNDWA "

Mradi wa DART ni mradi ambao unalenga kutoa huduma ya mabasi ya mwendo haraka, huu ni mpango unaotekelezwa kwa awamu 6 ambapo utakuwa umelifikia jiji lote la Dar es salaam.

Mradi unatekelezwa kwa ubia katika ya SERIKALI na SEKTA BINAFSI, yaani Public Private Partnership (PPP) kwa maana hiyo inatumika sheria ya PPP na kuna upembuzi yakinifu (Feasibility study) wa mradi huu ulioidhinishwa na Waziri wa Fedha na Mipango. Kwa ujumla Serikali inajenga miundombinu ya Bus Rapid Transit (BRT) na kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza kwenye huduma ya mabasi.

Hivyo Serikali (DART) iliingia makubaliano ya mpito (interim service agreement) na UDART kwa kuwa miundombinu ilikuwa imekamilika na ilianza kuvamiwa na wafanyabiashara/magari nk. Katika makubaliano hayo UDART anatoa huduma ya usafiri wa mabasi na kukusanya nauli na kuilipa serikali Access Fee. Katika hii ya kukusanya nauli UDART iliingia mkataba na MAXCOM kukusanya nauli kwa kutumia Automated Fare Collection System ambayo inahitaji utaalamu specialized wa ICT.

Sekta binafsi ni wafanyabiashara na wana interests zao kubwa kujihakikishia anapata faida. DART inazingatia huduma bora itolewe na mkataba una provision ya kufanya makato iwapo kuna huduma haikidhi vigezo kwenye mkataba. Vigezo vikubwa vinajumuisha "PANCTUALITY" na "AVAILABILITY".

KUHUSU NAULI :

Mkataba wa UDART na MAXCOM uliisha na UDART waliamua kutoendelea na MAXCOM. Suala hili limepelekea kuathiri huduma ya ukataji tiketi mpaka kutumika tiketi zisizo za kielektroniki. Inasemekana DART imeingilia kati kuhakikisha suala la UDART na MAXCOM haliathiri huduma na ukataji tiketi kwa kutumia tiketi za mfumo umerejea huku juhudi zikiendelea kumaliza suala lao ‘smoothly’.

MUUNDO WA BRT :

Mradi wa BRT ni mradi wa PPP kama nilivyoandika hapo juu ambapo serikali inajenga barabara na vituo, upande wa private kunakuwa na BUS OPERATOR (UDART ) ananunua mabasi na kuyaendesha , FARE COLLECTOR ananunua mitambo ya ticket / kadi na kutoa huduma ya tiketi na mtoa huduma mwingine ni FUND MANAGER hii ni benki ambayo imepwwa jukumu la kuweka fedha za mradi na kuwalipa watoa huduma.

WADAU SHIRIKISHI :

Kutokana na ukubwa na unyeti wa mradi kumekuwa na wadau mbalimbali wanaoshirikishwa nao ni :

- SUMATRA (leseni, viwango vya nauli)
- eGA (masuala ya ICT)
- POLISI (usalama vituoni, barabarani, kuna askari wapo assigned kwenye mradi)
- TANROADS (miundombinu ikiwemo ujenzi unaotarajia kuendelea Mbagala, Gongo la Mboto, Tegeta, Park & ride facilities)
- Manispaa (miundombinu ya barabara, park & ride facilities, maeneo ya karakana/vituo vikuu)
- TTCL (back office - kuhifadhi mfumo wa AFCS/ITS, internet)
- DAWASCO (maji safi/taka), TANESCO (umeme)
- NMB (Fund Manager) UDART (ISP)
- Wizara ya Fedha (masuala ya Fedha, PPP, Msajili Hazina, Fedha za fidia, GePG, OC, Salaries)
- Wizara ya Ardhi (Fidia, Mthamini)
- OR TAMISEMI (Wizara Mama wa DART
- TARURA), Wizara ya Ujenzi (Miundombinu, TANROADS)
-TRA (kodi)
-TAA/TCCA (njia ya Gongo la Mboto)
- DPs (World Bank, AfDB)
-Vyama vya wamiliki wa dala dala (UWADAR, DARCOBOA - very sensitive group needing great care of their issues)
- Wafanyabiashara wadogo wadogo
- Chama cha Walemavu
- OR-UTUMISHI (Wafanyakazi)
- CRB (Bodi ya wakandarasi)
- ERB (Bodi ya wahandisi)
- TBA (majengo)
- Ofisi ya Waziri Mkuu (Msimamizi mkuu wa yote)

MIPANGO :

- Mipango inayoendelea ni kuanza ujenzi wa awamu zinazofuata, njia ya Mbagala (mwaka huu), Gongo la Mboto (mwakani), na Tegeta (mwakani) kwa kuwa fedha zimepatikana na usanifu ndio unaofanywa kwanza. Pia kutakuwa na CONTOL CENTRE ambayo itasimikwa na kuangalia awamu zote 6, kuwekwa CCTV CAMERA vituoni na barabarani, kuwekwa SCREEN KWENYE VITUO kuonyesha taarifa ikiwemo MUDA basi litafika nk.

- Ikiwa zabuni zitaenda vyema, mabasi takribani 165 yataongezwa, mkusanya nauli ataleta kadi na zitaongezwa njia feeder 9.Kwa saaa zipo za Muhimbili na Mbezi-Kimara.

Zinazotarajiwa kuongezwa zitakwenda Masaki, Sinza, Chuo Kikuu, Mabibo na Kawe.

- Mpango wa kuboresha signals na kwa ujumla traffic management inakuja ambapo kutakuwa na Control room itakayosimikwa na humo masuala ya traffic management yamo ambapo itamuwezesha mtu kutoka Control room kuweza kusimamia flow ya traffic kwa kuwa ataona mfumo mzima.

- Kuna suala la PIS Public Information System ambayo itakuwepo pia. Kwa ujumla na huge ICT package na itakuwa state of art technology. Inatarajiwa hata Polisi watatumia facilities za CONTROL ROOM kuona AJALI (kubaini sababu nk) na KU-MONITOR hali ya usafiri.

Ndugu zangu wapendwa, hakika si jambo rahisi kama ilivyo kwa umiliki wa Daladala.....huu mradi wa mwendokasi ni vyema tukajua ni PILOT (SHAMBA DARASA) ambalo tayari limepata na Tuzo lakini hilo halisababishi kukosa kasoro ndogo ndogo.

Baada ya kusoma hapo juu maelezo kutoka kwa wadau naamini utaunga mkono juhudi hizi za kupunguza adha ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam.

Nashauri kwa wote ambao wana ushauri wa kiufundi (technical) ambao wanadhani utapelekea kuongeza UFANISI (efficiency) na KURIDHIKA kwa wateja (Customer satisfaction) kuwasiliana na mamlaka husika ili kwa pamoja tuijenge Tanzania yetu pendwa.

NOTE : Nukuu kutoka vyanzo mchanganyiko.

=====TUOMBE =====

MUNGU Ibariki Tanzania
MUNGU wabariki wenye mamlaka
MUNGU wabariki wana wa Tanzania

===== AMEN =====

Godwin D. Msigwa
Dar es salaam
Tanzania
29 Aprili 2018
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: