Friday, April 6, 2018

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MPWAPWA KIBARUA CHAOTA NYASI

Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Maje kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tamisemi Mussa Iyombe inasema Maje amesababishia hasara serikali ikiwamo kushindwa hata kukusanya mapato ya serikali.

“Hata makusanyo ya mwaka huu hatujui anapeleka wapi hadi leo amekusanya asilimia 24 tu katika halmashari ya kongwa na Mpwapwa licha ya kuwa na vyazo vingi vya mapato.

Iyombe amesema Mkurugenzi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu