Katika kusherehekea Pasaka nawaomba Wakristo wenzangu tutumie Damu Takatifu ya Yesu Kristo kuondoa kila namna ya uadui miongoni mwetu (ndoa, familia, hadi Taifa).

Waefeso 2:13-16

 “Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa Damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye AMANI yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha KUUONDOA ule UADUI kwa MWILI WAKE ; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu  mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya AMANI

... AKAWAPATANISHA wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya MSALABA, akiisha kuufisha ule UADUI kwa huo MSALABA”

Ni ukweli usiopingika kuwa Taifa letu lina makundi makubwa matatu ambayo lazima tuyanenee na kuyaondoa kupitia DAMU Takatifu ya Yesu Kristo na kuondoa viambaza vya UADUI .

1. Makundi mawili ndani ya dini:-

- Wanaouunga mkono waraka.

- Wanaoupinga waraka

2. Makundi mawili ndani ya Siasa

- Kundi linalounga mkono waraka

- Kundi linalopinga waraka

3. Kundi ambalo halipo upande wa siasa wala dini (HAWA NI WENGI).

Hivyo basi kupitia Damu Takatifu ya Yesu Kristo tumuombe MFALME WA AMANI aunganishe makundi haya yote hatimaye tushi kama ndugu huku tukichukuliana kwa namna yote huku kila mmoja akitimiza wajibu wake bila kuingiliwa.

Kauli ya Rais wa JMT John Pombe Magufuli aliyoitoa siku ya leo wakati wa Pasaka imesisitiza mambo makubwa manne:-
✍ Amani
✍ Upendo
✍ Kushiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa
✍ Matendo mafu yaani yaliyokufa au yasiyofaa yafufuke na kuwa matendo mema.

Ni wakati sahihi sasa kutumia Damu Takatifu ya Yesu Kristo kuliombea Taifa letu. Aidha upatano miongoni mwetu. Hasa viongozi wa dini na wanasiasa. Hapa hakuna mshindi bali MASLAHI MAPANA YA TAIFA YAWEKWE MBELE.

Mungu akubariki unaposhiriki maombi haya ya kufunga na kuomba ambayo yatahitimishwa tarehe 17/4/2018

Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Mathayo 5:9

“Lakini namna hii haitoki, ila kwa kusali na kufunga”. Mathayo 17:12

“Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” Mathayo 17:20

PASAKA NJEMA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: