Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Baada ya kupoteza mchezo wa kombe la Azam Sports HD Federation Cup dhidi ya Singida na United hatimaye nahodha wa timu ya Yanga afunguka na kutoa ya moyoni.

Kwa sasa Yanga wapo mkoani Morogoro wakijiandaa na mchezo wa kimataifa wa kombe la Shirikisho barani Afrika, nahodha Nadir Haroub Cannavaro’ amesema kuwa nafasi ya ubingwa bado wanayo kwani mechi hazijaisha.

Canavaro amesema kwa sasa kinachotakiwa ni wanachama kwa pamoja na umoja wao kuendelea kutoa hamasa na kuwapa moyo wachezaji ili waweze kufanya vizuri.

"Ni kweli tumepoteza mchezo wetu dhidi ya Singida United ambao ulikua ni muhimu kwa ajili ya kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa ila muda huu sio wa kuanza kukata tamaa kwani nafasi ya ubingwa bado ipo kuna mechi takribani 9 zimesalia," amesema Canavaro.

“Tunamsukuru Mungu tumefika salama Morogoro, tunawaomba mashabiki wa Yanga wasife moyo kutokana na kupoteza mchezo wetu dhidi ya Singida United japo tulijitahidi lakini tukafungwa kwa penati.”

Canavaro amewaonba wanachama kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi, na kuwaomba mashabiki waende kwa wingi kutupa sapoti ili tuweze kufanya vizuri.”

Kwa sasa Yanga imeweka kambi mjini Morogoro kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya waethiopia.

Yanga inatarajia kukutana tena na Singida United katika mchezo wa ligi kuu April 11 utakaofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: