ofisa wa TMA ambaye nesi Prisca Mwandaji akiongea na wananchi wakati wa ufunguzi wa zoezi la upimaji wa magojwa yasioambukiza na yale yanayoambukiza hususa ni upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu Pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi(HIV)ili kuwasaidia wananchi wa monduli Kujua afya zao.
Mmoja wa daktari kutoka chuo cha kijeshi monduli akiwa anampa ushauri mmoja wa mama wa kimasai aliyehudhuria kupima afya yake
Madaktari kutoka chuo cha kijeshi cha monduli (TMA) wakiwa wanatoa huduma ya upimaji wa magojwa yasioambukiza na yale yanayoambukiza hususa ni upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu Pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (HIV) bure ili kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Monduli.
Kaimu mganga mkuu halmashauri ya wilaya ya Monduli, Sakina Msangi akiongea na wananchi walioudhuria kupima.
Na Woinde Shizza, Monduli.

Zaidi ya wananchi 470 tarafa ya mto wa mbu wilayani monduli mkoani Arusha wamepatiwa huduma ya upimaji wa magonjwa yanayoambukiza na Yale yasioambukiza bure ili kuwawezesha wananchi hao kutambua afya zao

Huduma hiyo ambayo inatolewa na madaktari kutoka Katika chuo cha kijeshi cha monduli (TMA) inatarajiwa kuwafikia wananchi waliopo Katika kata, Tarafa na vijiji vyote vya wilaya ya Monduli.

Akizungumzia zoezi hilo Katika viwanja vya mto wa mbu ofisa wa TMA ambaye ni nesi Prisca Mwandaji alisema kuwa wao Kama madaktari kutoka chuo cha kijeshi cha monduli (TMA) wameamua kutoa huduma hii ya upimaji WA magojwa yasioambukiza na yale yanayoambukiza hususa ni upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu Pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi(HIV)ili kuwasaidiawananchi wa monduli Kujua afya zao.

"Hii ni moja ya kazi zetu wanajeshi kusaidia wananchi hivyo basi Susi kama madkatari tumeamua kujitoleakupima wananchi bure hawachangii hata kidogo na huduma hii tunaitoa katika tarafa zote za wilaya ya monduli na magonjwa ambayo tunapima na kushuri wananchi wanaokuja hapa kupima ni HIV Pamoja na kifua kikuu maana haya nimgonjwa mabaya na yanayoambukiza hivyo ndio maana tunawasisi tiza wananchi wapime ili wajue afya zao ukiangalia na huduma tunatoa bure"alisema Mwandaji.

Aidha alisema Kuwa hadi sasa walishapima tarafa Moja ambayo ni makuyuni ambapo jumla ya wananchi 350 na pia hapa mto wa mbu tumeshapima wananchi 470 na bado wanaendelea kuwapima.

"Kwakweli kwa upande WA muitikio ni mkubwa maana kwanza hadi sasa kwa hapa mto wa mbu tulishapita malengo tulitarajia kupima watu 450ila tumeshapita adi sasa tumeshapima watu 470 na tunaendelea hivyo kwakweli muitikio ni mkubwa mno kiukweli "alisema Mwandaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: