SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limetangaza kuanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo serikalini (GePG), ambao linasema utaliwezesha kuokoa takriban Sh. milioni 200 kila mwezi.

Mfumo huo umetajwa kulinufaisha shirika hilo kwa sababu utaondoa ulipaji wa tozo za kamisheni ya asilimia nne kwa kila muamala wake, ambayo awali ilikuwa ikilipwa kwa mawakala wakiwamo Maxcom na Selcom.

Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja wakati akitangaza mfumo huo kuanza kutumika kwenye malipo yote ya ankara za maji kuanzia leo.

Alisema wateja watalipia kwa kutumia huduma za kifedha kwa simu za mkononi za M-Pesa, tiGo Pesa na Airtel Money.Luhemeja alisema GePG ni mfumo wa serikali ambao unaunganisha taasisi zote za umma zinazotoa huduma na mteja wa huduma husika moja kwa moja, bila kuwepo mtu wa kati.

"Katika mfumo huu mpya," alisema Luhemeja, "malipo yatafanyika kwa kutumia kumbukumbu namba, yaani Control Number ambayo ina tarakimu 12 na tutakuwa tunaitoa kwa mteja, ili itumike kwenye malipo hayo kwa miamala ya kifedha kwa njia ya simu."

Alisema zaidi: "Shirika litapata fedha zake kwa wakati, kwa sababu zitakuwa zikiingia moja kwa moja kwenye akaunti yetu ya makusanyo na zitakazokuwa zimeokolewa kutokana na kupungua kwa gharama ya uendeshaji tutazirudisha kwenye utoaji huduma.

"Kwa utaratibu huu, DAWASCO haitohusika kwenye kulipia kamisheni ya miamala itakayokuwa ikifanyika na badala yake, mteja atakuwa anakatwa kiasi kisichopungua asilimia moja ya kila miamala ya malipo atakayofanya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: