Sehemu ya wachezaji wa timu ya Simba Sports Club wakifuatilia mjadala wa kipindi cha maswali na majibu wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
Viongozi wa timu ya Simba Sports Club wakifuatilia mjadala wa kipindi cha maswali na majibu wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Tulia Ackson, Baadhi ya Naibu Mawaziri na Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya Simba Sports Club wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso wakiwa katika picha ya pamoja na mshambuliaji wa timu ya Simba Sports Club Bw. Emmanuel Okwi (kushoto) wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai. Picha zote na Octavian Kimario wa WHUSM.
---
Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania bara (VPL) mwaka 2017/18, timu ya Simba leo wameliteka Bunge jijini Dodoma.

Mabingwa hao pamoja na benchi la ufundi na viongozi mbalimbali wa timu hiyo, wametembelea Bunge baada ya kupata mwaliko wa Spika Job Ndugai.

Hata kabla hawajatambulishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga, Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda alianzisha 'shangwe' bungeni humo.

Ilikuwa hivi, kabla ya Kakunda kujibu swali la Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Almas Maige, Naibu Waziri huyo ameanza kwa kusema, leo Mei 14, 2018 ameamka saa 10 alfajiri kujiandaa kujibu maswali lakini kubwa ni furaha ya ubingwa.

Huku wabunge wakishangilia, Kakunda akiwa mwenye furaha akasema,"Sasa naamini Watanzania watapata wawakilishi wazuri wa michuano ya kimataifa, hawatatupa presha."

Kakunda muda wote wa kujibu maswali ya wabunge amekuwa akichombeza maneno ya furaha ya ubingwa wa Simba na uwapo wao bungeni.

Hakuwa Kakunda pekee, bali hata Mbunge wa Ilala (CCM), Azzan Zungu aliposimama kuuliza swali la kujua mikakati ya kuboresha michezo kwa vijana na akaanza kwa kusema:

"Humu ndani kaingia mnyama mkali sana, lakini tuko salama," na shangwe kuendelea ukumbini.

Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubereje naye kabla ya kuuliza swali amewapongeza Simba akisema wamefanya kazi kubwa sana kuchukua ubingwa hata kabla ligi haijaisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: