Mwakilishi wa kikundi cha wazee cha Tumaini Kilenzi akipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili kutoka kwa Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda akifafanua kwa wawakilishi wa vikundi vya walemavu na wazee wakati wa makabidhiano ya msaada wa shilingi milioni nane kwa vikundi vya walemavu na wazee.Kushoto kwake ni Afisa Ustawi Mji Njombe Hosea yusto akifatiwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt. Thomas Samwel Ndalio.
Sehemu ya wawakilishi wa vikundi vya walemavu na wazee waliofika kwenye makabidhiano hayo.
Mwenyekiti wa Walemavu Mkoa wa Njombe Ndg. Sianga akipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kikundi cha Duka la Walemavu Njombe.

Hyasinta Kissima - Njombe.

Halmashauri ya Mji Njombe imetoa misaada yenye thamani ya shilingi milioni nane kwa vikundi vinne vya walemavu na wazee lengo ikiwa ni kuinua mitaji ya shughuli zao za maendeleo bila masharti yoyote.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa Halmashauri imetenga kifungu maalumu kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu na itaendelea kuwasaidia kwa kadri wanavyoendelea kufanya vizuri.

“Naomba mfahamu kuwa mpaka kufikia sasa Halmashauri imekusanya mapato kwa asilimia 91% na mapato haya ndio yamewezesha leo hii kuweza kuwapatia fedha hizi. Hizi fedha ni za kwenu, tunakusanya kutoka kwenu na lazima tuzirudishe kwenu. Hivyo naomba tushirikiane katika zoezi la ukusanyaji mapato na pia kupitia ninyi mkawe waalimu na wahamasishaji wazuri wa ukusanyaji mapato ya Halmashauri hususani kwa wale wanaobeza zoezi zima la ukusanyaji mapato ya Halmashauri na serikali kwa ujumla.”Alisema Mwenda.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt. Thomas Samwel Ndalio amesema kuwa lengo la vikundi hivyo vya maendeleo vilivyoundwa ni kwa ajili ya kujikwamua wenyewe kimaendeleo lakini pia kuondoa dhana iliyojengeka kwenye jamii kuwa mlemavu hawezi kufanya shughuli za maendeleo.

Aidha Dkt. Thomas amesema kuwa Halmashauri imetambua uwepo wao kwa kukubali kufanya shughuli zinazowatambulisha wao katika jamii na kuweza kutenga bajeti na kuvishauri vikundi hivyo kuhakikisha kuwa wanafungua akaunti rasmi za vikundi katika taasisi za kifedha.

Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu Mkoa wa Njombe ameishukuru idara ya afya kupitia Ustawi wa Jamii na kusema kuwa kwa zaidi ya miaka thelathini akiwa kama kiongozi wa walemavu hajawahi kushuhudia jambo kama hilo likifanywa na Halmashauri na hii ni mara ya kwanza kwa Halmashauri kuwaunga Mkono na amempongezi Mkurugenzi kwa kunyoosha mkono wake na kuwasaidia.

“Zaidi ya miaka thelathini nikiwa maka Kiongozi wa walemavu sijashuhudia jambo kama hili hivyo Ndugu zangu sidhani kama kuna mtu atachukua fedha hii na kufanya nje ya utaratibu maana nafahamu serikali inaweza kukutembelea muda wowote na watakapofika wakaona tunachofanya ni sifuri watavunjika moyo kuna wenzetu hawajapata msaada huu hivyo inabidi tutangaze kuwa tumewezeshwa” Alisema Fianga

Vikundi vilivyopatiwa msaada huo ni pamoja na Kikundi cha Wazee Tumaini Kilenzi, Duka la walemavu Njombe, Kikundi cha Wasiiona Njombe (UVIWANJO) na Chama cha Wasiosikia Njombe( CHAVITA).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: