Monday, May 14, 2018

MSANII LULU MICHAEL KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE

Muigizaji Elizabeth Michael, maarufu Lulu leo Jumatatu Mei 14, 2018 amebadilishiwa adhabu na sasa anatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Magereza imethibitisha kuhusu uamuzi huo.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.

Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ambaye baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa upande wa mshtakiwa alitoa hukumu.

Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mpenzi wake.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu