Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya ambaye alikuwa mgeni rasmi (wa tatu toka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili toka kushoto) wakikata utepe wa kuzindua huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wagongwa wakipata huduma ya  kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo ilipofanyika uzinduzi katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.

Mmoja ya madaktari alionyesha mashine ya kusafisha damu.
Mkuu wa kitengo cha huduma ya  kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo Dkt. Paschal Ruggajo (mwenye nguo nyeupe) akitoa ufafanuzi juu ya huduma wanayoitoa katika kitengo hicho.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika uzinduzi wa huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika uzinduzi wa huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma za Hospitali Prof. Said Aboud akizungumza katika uzinduzi wa huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (katikati) wakifurahia jambo wakati Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma za Hospitali Prof. Said Aboud alipokuwa amesimama kwenda kutoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi na wanafunzi waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi na wanafunzi waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa maelekezo kwa watendaji wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Picha ya pamoja.
Mkuu wa kitengo cha huduma ya  kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dkt. Paschal Ruggajo (mwenye nguo nyeupe) akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza uzinduzi iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya amezindua huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MAMC.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hizi, Dr. Mpoki amesisitiza umuhimu wa huduma hii kwa kutoa takwimu zinazoonyesha ongezeko la magonjwa ya figo kwa kasi kubwa duniani hususani katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

"Inakadiriwa kuwa kuna wagonjwa 7-10 wa figo kwa kila watu 100 na kwamba ifikapo mwaka 2030, katika kila wagonjwa 100 wa figo duniani, wagonjwa 70 watakuwa ni wakazi wa ukanda huo ikiwemo Tanzania", alisema. Katibu Mkuu aliendelea kueleza kuwa kitengo hiki cha kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo cha MAMC kina jumla ya mashine 12, na hivyo kina uwezo wa kuhudumia zaidi ya wagonjwa 10,000 kwa mwaka, wakiwemo wasio na maambukizi na wenye maambukizi. 

Amesema kitengo hiki pia kitatoa mafunzo endelevu kwa madaktari wajao na kitakuwa chachu ya tafiti zenye kutoa miongozo ya matibabu na kuboresha sera za matibabu ya magonjwa ya figo nchini.

Aidha, Dr. Mpoki ameupongeza uongozi na wafanyakazi wote wa MAMC kwa maendeleo makubwa yaliyopatika katika kutoa huduma kwa wananchi na kufundisha wataalamu bingwa katika fani za afya katika kipindi cha miezi sita tu tangu Hospitali ilipofunguliwa rasmi mwishoni mwa mwezi Novemba 2017.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo alisema mafunzo rasmi ya madaktari bingwa wa magonjwa ya figo Tanzania yalianza mwaka 2007 katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Bergen (Norway) na Chuo Kikuu cha CMC-Vellore (India) kupitia ufadhili wa Serikali ya Kifalme ya Norway. Mpaka sasa, Dkt. Akwilapo amesema madaktari bingwa wa magonjwa ya figo kumi wamehitimu hapa MUHAS, kati ya hao wanane toka Tanzania, moja toka Uganda na mmoja toka Ethiopia.

Dkt Akwilapo alisema pamoja na mafunzo yanayotolewa tafiti katika magonjwa ya figo ni muhimu katika kungàmua vyanzo vya magonjwa ya figo na kutoa miongozo ya mwelekeo wa matibabu ya figo nchini. Kutokana na hilo, Dkt. Akwilapo amesema Kitovu cha Tafiti za Magonjwa ya Figo Tanzania (Renal Research Group) sambamba na huduma za biopsia ya figo pia zitazinduliwa leo katika Hospitali hii ya MAMC.

Akieleza kuhusu kupanuka kwa huduma za MAMC, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema tangu hospitali ilipoanza kutoa huduma tarehe 18 Septemba, 2017 mpaka mwishoni mwa mwezi Aprili 2018, jumla ya wagonjwa 20,250 wa kliniki za nje na wagonjwa 1,785 wa kulazwa wamehudumiwa. 

Prof. ameshukuru juhudi kubwa za Serikali kuhakikisha huduma bora za matibabu ya kibingwa ya rufaa zinapatikana kwa wingi nchini na pia juhudi za wafanyakazi wote wa MAMC katika kufanikisha jitihada hizi za Serikali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: