Thursday, May 10, 2018

PROF. MWANDOSYA, NAPE WATOA NENO ZITO KWA MBUNGE JOSEPH MBILINYI 'SUGU' BAADA YA KUTOKA GEREZANI

Waziri wa Serikali ya Awamu ya Nne, Profesa Mark Mwandosya na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye wamemkaribisha uraiani mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu aliyetoka gerezani leo Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais John Magufuli.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook, Profesa Mwandosya ambaye aliambatanisha na picha akimpa mkono mbunge huyo amesema,”nikimpa hongera mbunge wangu wa Mbeya Mjini kwa kuhitimu chuo cha uanasiasa Gereza la Ruanda Mbeya leo Mei 10, 2018.”
Mwandosya ambaye aliambatana na mkewe alipokwenda nyumbani kwa mbunge huyo katika andiko lake hilo amefafanua zaidi, “Somo, kutofautiana vyama, itikadi na misimamo isiwe msingi, uhasama na uadui. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, Ibariki Tanzania.”

Huu ni ufafanuzi zaidi walioutoa Jeshi la Magereza juu ya msamaha wa Sugu;
Kwa upande wake Nape kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika, “karibu tena uraia brother (kaka). Nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo ulipoanza siasa.”

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu