RAIS wa Zimbabwe, Mhe Emmerson Dambudzo Mnangagwa (mwenye skafu) akiwa na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) wa CCM, Comrade Ngemela Eslom Lubinga (katikati mwenye miwani) pamoja na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo Ndugu Zitto Zuberi Kabwe (anayemweleza jambo Rais Mnangagwa) pamoja na washiriki wengine wa mkutano wa Zimbabwe Center for Democracy (ZCD) uliomalizika leo katika Hotel ya Elephant Hills, Victoria Falls leo.

Rais Mnangagwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa ZANU-PF, alihudhuria mkutano huo na alitoa shukrani nyingi kwa ujumbe wa Tanzania kwa kuwapa elimu na uzoefu mzuri utakaowasaidia kufanya uchaguzi wa kidemokrasia kwa amani na utulivu.

Ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ulijumuisha vyama vitatu vya siasa vya CCM, NCCR MAGEUZI na ACT Wazalendo.

Mhe Mnangagwa ni Rais wa pili wa Zimbabwe tangu wapate uhuru mwaka1980 kutoka kwa utawala wa walowezi. Pichani, Rais Mnangwaga akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, baada ya kuufunga rasmi leo (Mei 14, 2018) katika hoteli ya Elephant Hills, Victoria Falls, Zimbabwe.

Wazimbabwe wanategemea kufanya uchaguzi wao Mkuu baadaye mwaka huu (2018) ambapo Rais Mnangagwa anatarajiwa kupata ushindi wa kishindo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: