Wakwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambae ni mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi ,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,,Katibu tawala wa Jiji la Arusha Charles Kwitega na Karibu wa Tughe Jijini hapo Samweli Magero.Picha Vero Ignatus Boog.
Meza kuu wakiwa wanafurahia jambo wakati wakati Maandamano ya wafanyakazi yakiingia uwanjani .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka kiwanda cha A-Z wakiwa wanapita mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za meimosi katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha Jijini Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abaid bado wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali waliendelea kusalia uwanjani bila kuondoka katika sherehe za Mei Mosi mkani hapo. Picha na Vero Ignatus Blog.
Fedy Sanga( kulia)akikabidhiwa cheti na Hundi ya Sh, milioni 1 baada ya kuteuliwa kuwa mfanyakazi bora Kwa wafanyakazi wa Jiji la Arusha. Picha na Vero Ignatus Blog.

Na Vero, Ignatus, Arusha.

Mkuu wa mkoa mrisho Gambo amewataka waajiri kupokea changamoto za wafanyakazi na kuzitatua sambamba na wafanyakazi kuwa huru kusema changamoto wanazokumbana nazo.

Gambo amekemea kitendo cha baadhi ya waajiri wanaowatisha wafanyakazi,amesema kuwa jambo hilo halikubaliki, atakapobainihatua stahiki zitachukuliwa.

"Nimepata taarifa kuna maeneo ambayo wafanyakazi waliweza kutoa kero zao na maoni yao na baadhi ya waajiri waliwatisha ,jambo hilo halikubaliki na atakapobainika sheria stahiki zitachukuliwa dhidi yake" alisema Gambo.

Ameyazungumza hayo katika sherehe za mei mosi Jijiji Arusha ambapo alikuwa mgeni rasmi na kutilia mkazo kuwa yapo malalamiko ya watumishi wa serikali kukamatwa na kuwekwa ndani kwa makosa ambayo ni ya kiutumishi,amewataka viongozi kufanya kazi kwa weledi,kwakuzingatia sheria na taratibu.

"Kama mfanyakazi amefanya kosa la kiuhalifu,ashughulikiwe kama mhalifu,bali kama kosa ni la kiutumishi, zipo sheria na kanuni za kitumishi ni vyema zikazingatiwa"

Amesema wafanyakazi wanatakiwa kuwa na ujasiri wa kufanya kazi kwani viongozi pekee wa mkoa hawawezi kusukuma gurudumu la maendeleo bila ya kushirikuana na wafanyakazi ambao ni wadau muhimu katika nchi.

Akijibu risala ya wafanyakazi Jijini Arusha iliyosomwa na Katibu wa Tughe Samweli Magero amesema kuwa changamoto ya uhaba wa majaji tayari mhe.Rais alifanya uteuzi wa majaji kadhaa ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kwenda kuziba mapengo yaliyokuwepo.

Mwisho aliwapongeza wananchi kwa ujumla pamoja na wafanyakazi kuwa wameweza kuonyesha uzalendo kwa mkoa kwani Arusha imebadilika kwa kuithamini amani kuliko chochote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: