Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ujenzi wa Stendi ya mabasi ya kwenda mkoani kinatachotarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa standi hiyo ya kisasa inayotarajiwa kujengwa ambayo itakuwa na sehemu za kupumzikia abiria,itakuwa na sehemu za kupaki magari madogo takribani 300,pamoja na Mabasi makubwa 200,na sehemu za biashara. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).
Baadhi ya watendaji wa Manispaa wakisikiliza mjadala uliokuwa ukiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
---
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezungumza na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya watendaji hadi wakurugenzi wa Manispaa kuhusu miradi mbalimbali ya kichumi katika kujenga nchi.

Makonda ameeleza hayo leo wakati anzungumzia ujenzi wa Stendi ya mabasi ya abiria yaendayo mikoani Ubungo ambao tayari Sh. bilioni 50 imetolewa kwa ajili ya kuanza kujengwa kituo hicho kitakachokuwa cha kisasa kikiwa na huduma mbalimbali za jamii ikiwemo hoteli, supermarketi na huduma za kibenki.

Makonda ameeleza kituo hicho kinatarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Luis ambapo amebainisha Manispaa za Jiji hilo imetengewa bajeti ya Sh. bilioni 250 kutoka Mfuko wa Rais kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali.

Pia amesema miradi inayosimamiwa na Manispaa ambayo Serikali inaifanyia kazi kama fukwe ya Coco beach ambayo ni mali ya wananchi na itatengenezwa ili wananchi wafurahi kutembelea na kushiriki kula keki ya taifa.

Aidha ameongeza kuwa mapato yameongezeka kutoka Sh.milioni 87 hadi Sh. bilioni moja na kuwasisitiza watendaji kuwa wakali kuhusu matumizi ya fedha.

Makonda amesema lazima manispaa zote ziwe na uchumi madhubuti na kuwahudumia wananchi na kuiacha Serikali kuu kujenga miradi mikubwa kama Standard gauge, miradi ya umeme sambamba na kuangalia usalama nchini.

Pia amewataka wananchi wa Mkoa huo kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kazi kubwa ya kuleta mabadiliko nchini na ameahidi kama watendaji watashirikiana katika kuifikisha Tanzania katika maendeleo na kueleza kuwa haina haja ya kumbeza Rais Magufuli kwani kazi anayoifanya ni kwa faida ya wananchi kama vile miradi ya maji, barabara na umeme hivyo lazima tutambue mchango huu na tuunge mkono juhudi zake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: