Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akiimba wimbo wa Mshikamano Daima pamoja na meza kuu kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe zaidi ya 190 wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima wakati wa Mkutano wa Baraza hilo Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katikati walio kaa, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara hiyo walioshiriki Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma, kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Cyprian Kuyava.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (kushoto) na Mhasibu Mkuu wa Fungu 21 wa Wizara hiyo Bw. Sayi Nsungi, wakifuatilia majadiliano wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Wajumbe Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiendelea na Mkutano Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango).
---
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuongeza ukusanyaji wa mapato na kusimamia nidhamu ya matumizi ya Fedha za Umma ili kuijengea Serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi na kuifanya nchi iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Dkt. Mpango ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliowakutanisha wajumbe zaidi ya 190 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inajukumu la kuhakikisha inatekeleza usemi wa “Wizara ya Fedha na Mipango ndiyo Moyo wa Serikali” kwa kutumia Baraza la Wafanyakazi katika kushauriana na kuchangia mawazo yatakayosaidia katika kutekeleza majukumu ya Wizara kama yalivyopangwa na kusukuma kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

“Watumishi wote wa Wizara mnaowajibu wa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia utaalamu mlionao na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma ili kuongeza tija” alieleza Dkt. Mpango.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: