Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akizungumza wakati akifungua mashindano ya Vijana ya Banda Cup kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo pia alitoa vifaa vya michezo kwa timu zote 16 ambazo zinashiriki mashindano hayo.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Jezi mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Jezi mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoa na viongozi wa  timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo.
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akisalimiana na  wachezai wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup mara baada ya kuizundua na kugawa vifaa vya michezo.
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akisalimiana na  wachezai wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup mara baada ya kuizundua na kugawa vifaa vya michezo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto akiingia kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati alipokwenda kuzindua mashindano ya Banda Cup na kugawa vifaa vya michezo kwa timu 16 zinazoshiriki michuano hiyo kulia ni Meneja wa Uwanja wa CCM Mkwakwani

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 16 ambazo zinashiriki michuano ya Banda Cup ikiwa ni mchango wake kusaidia mashindano hayo.

Makabidhiano hayo yalifanywa kwa timu 16 ambazo zinashiriki mashindano hayo wakati alipokwenda kuyafungua kwenye viwanja vya CCM mkwakwani mjini Tanga.

Mashindano hayo yameanzishwa na Beki wa timu ya Baroka FC ya nchini Afrika kusini Abdi Banda akiwa na lengo la kusaidia kuinua vipaji vya soka na kuvikuza ili kuweza kuwa na hazina kubwa kwa siku zijazo.

Akizungumza juzi wakati akikabidhi vifaa hivyo ambazo ni Jezi seti mojamoja kwa kila timu shiriki,Waziri Ummy alisema mchezo wa mpira wa miguu unaweza kuwasaidia vijana iwapo watazingatia na kujituma.

Alisema pamoja na hayo lakini anampongeza muandaaji wake kwa kuona namna ya kuyaanzisha ili kuwasaidia kukuza vipaji vya wachezaji wachanga ambao baadae wataweza kusaidia kwenye soka letu.

“Nimempongeza kwa moyo wake wa uzalendo na sio kwamba ana fedha nyingi sana lakini kile kidogo anachokipata ameona ashirikiana na watuwa Tanga hivyo nasi tutahakikisha tunashirikiana naye”Alisema

Hata hivyo Waziri huyo alisema licha ya kutoa vifaa hivyo lakini atatoa fedha kwa Mfungaji bora 100,000, mwamuzi bora 100,000, timu yenye nidhamu 200,000, mlinda mlango bora 100,000 huku mchezaji bora akitoka na 100,000.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Ummy, Mratibu waMashindano Ibrahimu Kidiwa alisema katika mashindano hayoyanashirikisha timu 16 ambapo mshindi wa kwanza atapata sh.500,000,mshindi wa pili atapata 250,000,mshindi wa tatu atapatash.100,000 na mipira miwili (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: