Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

KLABU ya Yanga Sc kupaa leo kuwafata USA Alger Nchini Algeria katika hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wawakishilishi hao wa Tanzania ambao wanatarajia kucheza na USM Alger katika mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi kombe la shirikisho wanaondoka leo saa 11 jioni kupitia Dubai.

Kikosi hicho kinasafiri na wachezaji 20 pamoja na viongozi 8 wakiwepo na benchi la ufundi ambapo mtanange huo utachezwa nchini Algeria Mei 6 mwaka huu majira ya saa 4 Usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Yanga Jijini Dar es Salaam Msemaji wa kikosi hicho Dismas Ten amewataja baadhi ya wacheza ambao wapo katika msafara huo ni Rostand Youth,Ramadhani Kabwili,Gadiel Maiko,Obrey Chirwa, Pato Ngonyani, Kelvin Yondani, Ibrahim Ajibu.

Dismas Ten amesema Wachezaji hao ambao wapo kwenye msafara huo ni ambao wapo katika programu ya mwalimu,

"Tunaitaji matokeo maandalizi ya muhimu yameshafanyika ukizingatia tupo ugenini mchezo ni mgumu kikosi cha USM Alger kipo vizuri sio timu ya kibeza wapo kwenye michuano haya ya kimataifa kwa mudu mrefu"amesema msemaji huyo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: