Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda akizungumza na waandishi wa habari wakati wakuzindua promosheni ya mwezi mmoja ijulikanayo kama AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde ambapo wateja wa Airtel watajishidia zawadi kabambe pale wanapobet kwa kutumia Airtel Money. Kushiriki, mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kubet. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala SportPesa Tarimba Abbas.
 Mkurugenzi wa Utawala SportPesa Tarimba Abbas akizungumza na waandishi wa habari wakati wakuzindua promosheni ya mwezi mmoja ijulikanayo kama AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde ambapo wateja wa Airtel watajishidia zawadi kabambe pale wanapobet kwa kutumia Airtel Money. Katikati ni Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Isack Nchunda na Meneja Uhusiano Jackson Mmbando.
Mkurugenzi wa Masoko Isack Nchunda – kulia, Mkurugenzi wa Utawala SportPesa Tarimba Abbas – wa pili kulia, Sabrina Msuya Meneja Uhusiano SportPesa na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando wakionyesha baadhi ya zawadi ambazo wateja wa Airtel watashinda kwenye promosheni ya AMSHA AMSHA NA AIRTEL MONEY NA USHINDE ambayo ni ushirikiano wa Airtel na SportPesa.
---
Wateja kujishidia zawadi kwa kubet kupitia AMSHA AMSHA na Airtel Money Chezea kwa kutumia Airtel Money ujishindia zawadi kabambe kutoka SportPesa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na SportPesa imezindua promosheni ya mwezi mmoja ijulikanayo kama AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde ambapo wateja wa Airtel watajishidia zawadi kabambe pale wanapobet kwa kutumia Airtel Money. Promosheni hiyo ya Airtel Shida na SportPesa inaanza leo mpaka Julai 15 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema kuwa promosheni ya AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde inatoa nafasi nyingine kwa wateja wetu wa Airtel Money kuweza kujishindia zawadi kabambe kwa kubet kwa kutumia Airtel Money. ‘Airtel siku zote tunaleta huduma na bidhaa zenye ubunifu na za kutuweka karibu na wateja wetu. Tunaelewa ya kwamba michezo pamoja na mambo ya kubet imekuwa na maisha ya kawaida kwa wateja wetu. Kwa kuzindua promosheni hii ambayo tumeshirikiana na SportPesa inatoa nafasi nyingine ya kuendelea kutuweka karibu na wateja wetu’, aliongeza Nchuda.

Nchuda alisema kuwa promosheni itakuwa wazi kuanzia leo saa sita usikuna itaendelea kwa muda wote wa promosheni, ili kushiriki AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde

mteja wa Airtel Money anachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha anabet siku ambayo droo iko wazi na moja kwa moja namba yake itaingizwa kwenye droo ya wiki. ‘Mteja atatakiwa kubet siku ya droo ili kupata nafasi ya kuwa moja ya washindi, alisema Nchuda huku akiongeza kuwa wateja wanatakiwa kuhahakikisha kuwa wanayo pesa kwenye akaunti yao ya SportPesa.

Aliongeza kuwa kila droo ya kupata washindi wa AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde itachezesha wazi kwa usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania ambayo ndio wenye jukumu la kusimamia michezi yote ya bahati nasibu hapa nchini. Nchuda alitajwa zawadi za kila siku kama simu za smartphone, jezi za timu za Simba na Yanga pamoja na tiketi za kushuhudia mechi za Simba na Yanga kwa msimu mzima huku zawadi za wiki zikiwa ni TV yenye inchi 32 pamoja na ving’amuzi kutoka Star Times.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tarimba Abbas alisema kuwa droo ya kila siku na ya wiki za AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde zitakuwa zinachezezwa kwa pamoja kila wiki. ‘Airtel na SportPesa watakuwa wanatangaza majina ya washindi wa AMSHA AMSHA na Airtel Money na ushinde na kuchapisha majina yao kwenye magazeti, alisema Tarimba huku akiongeza kuwa washindi wa simu za smartphone, TV, jezi za Simba na Yanga pamoja tiketi za kushuhudia mechi za Simba na Yanga watatakiwa kuwa na vitambulisho vya kupiga kura, leseni ya udereva, pasi ya kusafiria au Barua kutoka serikali za mitaa kwa ajili ya utambulisho huku akiongeza kuwa mshindi hatatakiwa kulipa chochote kupata zawadi yake.

Aliongeza kuwa mteja atatakiwa kujiandikisha, kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kwa kutumia Airtel Money halafu ndio abeti. Mwisho wa kuchukua zawadi itakuwa ni Agosti 31 na zawadi hazitabidilisha kwa fedha, alisema Tarimba huku akiongeza kuwa washindi wanaweza kuchukua zawadi zao kutoka duka lolote la Airtel hapa nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: