Waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akimkabidhi Felista Elius pamba aliyovuna, wakati alipotembelea Kijiji cha Bukama kilichopo kata ya Mbutu Wilayani Igunga Mkoani Tabora akiwa safarini kuelekea Mjini Dodoma, Jana 17 Juni 2018. Picha zote Na Mathias Canal-WK

Na Mathias Canal-WK, Igunga-Tabora.

Waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba ameshtushwa na wanawake pekee kuwa kwenye mashamba wakivuna pamba ilihali waume zao wakiwa kwenye Chang’aa (Pombe za kienyeji) ama kwenye vijiwe kupiga soga.

Dkt Tizeba ameshtushwa na wanawake wengi kuwa shambani wakivuna pamba ilihali waume zao wakiwa kwenye vijiwe vya pombe za kienyeji mara baada ya jana 18 Juni 2018 kutembelea katika Kijiji cha Bukama na Mwakipoleja vilivyopo katika kata ya Mbutu Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora kujionea hali ya mavuno ya zao la pamba.

Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba amesema kuwa kwa muda mrefu imekuwa kama utamaduni wa kawaida kwa wanaume katika maeneo mengi nchi kuwatelekeza wake zao wakati wa kuvuna pamba lakini wakati wa mauzo wanawake hao huachwa nyumbani pasina kujua kiasi kilichopatikana baada ya mauzo.

Hata hivyo wananchi wengi ambao ni wakulima wa pamba kijijini hapo wameishukuru Serikari kwa kuweka mfumo mzuri wa ununuzi wa zao hilo, ambalo kwa mwaka huu linauzwa kupitia katika minada inayosimamiwa na Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS).

Pia wakulima hao wameiomba Serikali kuziwezesha AMCOS kuwa na maghala makubwa na ya kisasa ya kuhifadhia pamba, lengo likiwa ni kuhakikisha pamba inahifadhiwa kwenye maeneo salama na kuifanya isipoteze ubora.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: